У нас вы можете посмотреть бесплатно HOTUBA YA RAIS MAGUFULI 'AKIFUNGUA' MAKTABA YA KISASA UDSM (27/11/2018) или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Novemba, 2018 amefungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwl. Julius K. Nyerere) Jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati imejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na inakuwa maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika. Akizungumza katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Balozi wa China hapa nchini. Wang Ke na kumuomba apeleke shukrani za Tanzania kwa Rais wa China Xi Jinping kwa misaada ambayo China imekuwa ikiitoa kwa Tanzania, ikiwemo ujenzi wa Maktaba hiyo na Chuo cha VETA kitakachojengwa Mkoani Kagera. Rais Magufuli amesema urafiki wa China na Tanzania ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong umeendelea kuleta manufaa makubwa na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano na itauendeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano huu mzuri. “Jambo la kufurahisha ni kwamba misaada yao haiambatani na masharti. Wenyewe wakiamua kukupa wanakupa, walitujengea TAZARA, URAFIKI na pia wametusaidia katika maeneo mengine ya maendeleo” amesema Rais Magufuli na kumhakikishia Mhe. Balozi Wang Ke kuwa Serikali itahakikisha kila msaada unaotolewa unatumiwa vizuri. Aidha, Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mstaafu Prof. Rwekaza Mukandala kwa kuandaa mpango wa ujenzi wa maktaba hiyo, na pia amewapongeza Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kupata maktaba ambayo itawasaidia kuongeza kiwango cha ubora wa elimu. Katika taarifa yake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye amesema majengo ya maktaba hiyo yenye ghorofa mbili yamechukua eneo lenye ukubwa wa meta za mraba 20,000 yakiwa na uwezo wa kuhifadhi vitabu 800,000, kukalisha watumiaji 2,100 kwa wakati mmoja, yana kompyuta 160 zilizounganishwa na mtandao kwa ajili ya kusoma vitabu kwa njia ya kielektroniki, ofisi za wafanyakazi, eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum na ukumbi wa kisasa wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua watu 600. Prof. Anangisye ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa uliosaidia kufanikisha ujenzi wa maktaba hiyo, ameishukuru Serikali ya China kwa kutoa msaada wa fedha za ujenzi huo na kampuni ya ujenzi ya Jiangsu Jiangdu ya China kwa kujenga majengo yenye ubora na hadhi ya hali ya juu.