У нас вы можете посмотреть бесплатно JENGO MAARUFU MBULU MJINI "GUWANGW" LATEKETEA KWA MOTO | DEC 27 KUAMKIA DEC 28.2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MOTO WATEKETEZA NDOTO ZA WAFANYABIASHARA KATIKA JENGO MAARUFU LA GUWANGW, MBULU MJINI Ndoto za wafanyabiashara katika jengo maarufu la Guwangw, Mbulu Mjini, zimegeuka kuwa majivu baada ya moto mkubwa kuteketeza maduka yao usiku wa kuamkia tarehe 28 Desemba 2025. Miongoni mwa waathirika wa tukio hilo ni mfanyabiashara ndugu Mery Mazengo, ambaye amesema amepata hasara kubwa inayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 100. Akizungumza kwa uchungu, amesema amepoteza mali zote zilizokuwa katika duka lake la chini pamoja na duka la juu, huku baadhi ya mali zikiharibika wakati wa jitihada za uokoaji. “Nimepoteza kila kitu. Sina hata mtaji wa kuanzia upya. Tunaomba msaada kutoka serikalini na kwa wadau wengine ili turejee katika biashara, kwani tuna watoto tunaowasomesha,” amesema Mazengo. Kwa upande wake, ndugu Daniel Philopo, mfanyabiashara mwingine katika jengo hilo, amesema hasara aliyopata si chini ya shilingi milioni 60. Amesema hakuweza kuokoa kitu chochote kutokana na kasi ya moto. “Ni hasara tupu. Tunahitaji msaada ili kujikimu,” amesema. Akizungumza kama shahidi wa tukio, ndugu Patrice Isdori amesema chanzo cha moto kinahisiwa kuwa ni hitilafu ya umeme. Amesema kabla ya tukio, kulikuwa na shughuli ya kuchomelea mlango wa duka la wakala, na baadaye majira ya saa 4:00 usiku moto ulianza kuonekana katika eneo la paa la mbele ya chumba hicho. “Wananchi walijitahidi kuzima moto, lakini kulikuwa na changamoto kubwa ikiwemo uwepo wa mitungi ya gesi, huku moto ukisambaa kwa kasi,” amesema. Come TV Tanzania ilifanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, ndugu Michael Semindu, ambaye amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea pamoja na tathmini ya mali zilizoharibika. Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, ndugu Emanuel Tulinago Kibona, amesema walipokea taarifa za moto huo tarehe 27 Desemba 2025 majira ya saa 5:15 usiku. Baada ya kupokea taarifa hiyo, walifika eneo la tukio kwa haraka na kushirikiana na wananchi katika juhudi za kuzima moto. Amesema baada ya muda waliweza kudhibiti moto huo, ingawa kwa tathmini ya awali inaonekana kuwa hakuna mali iliyookolewa. “Moto ulikuwa mkubwa sana. Serikali ya mkoa inaendelea na mpango wa kununua gari la zimamoto ili kuimarisha uwezo wa kukabiliana na majanga kama haya. Tunatoa wito kwa wamiliki wa biashara kuwekeza katika vifaa vya tahadhari dhidi ya moto,” amesema Kibona. Jeshi la zimamoto limeeleza kuwa linaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo halisi cha moto pamoja na kufanya tathmini kamili ya hasara iliyojitokeza. Chanzo: Come TV Tanzania Mwandishi: Hussein Thabit Tarehe: 28 Desemba 2025