У нас вы можете посмотреть бесплатно Kilichojiri kesi ya padri na wenzake wanane tuhuma za mauaji ya Asimwe или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Watuhumiwa wanane wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath (2) wamefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba akiwapo Paroko Msaidizi Elipidius Rwegashora wa Parokia ya Bagandika wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera. Mtoto Asimwe alichukuliwa Mei 30, 2024 na watu wawili wasiyojulikana akiwa nyumbani na mama yake, saa 2:30 asubuhi katika Kitongoji cha Mbale kilichopo katika Kijiji cha Bulamula, Wilaya Muleba mkoani Kagera. Mabaki ya mwili wa marehemu Asimwe yalikutwa yametelekezwa kwenye mfuko wa sandarusi chini ya karavati katika Barabara ya Ruhanga Makongora, katika Kitongoji cha Malele, Kata Ruhanga, Juni 17, 2024 na kuzikwa siku iliyofuata Juni 18, 2024, nyumbani kwao. Washtakiwa wote tisa, leo Ijumaa Juni 28, 2024 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba na kusomewa shitaka moja la mauaji ya kusudiwa ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe, ambalo ni shauri namba 17740. Awali, Mkuu wa Mashtaka Mkoa Kagera, Waziri Magumbo amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, hivyo washtakiwa wote hawatakiwi kujibu chochote hadi watakapofikishwa Mahakama Kuu. Jamhuri imefungua shauri hilo la mauaji ya kukusudia namba 17740 la mwaka 2024 ambalo limesomwa na Mkuu wa Mashtaka Mkoa Kagera, Waziri Magumbo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Bukoba, Eliapokea Wilsoni, aliyesikiliza shauri hilo. Baada ya kutajwa kwa shauri hilo na kusikiliza na Hakimu Mkazi Bukoba, Eliapokea Wilson amehairisha kesi hiyo hadi Julai 12, 2024, shauri litakapotajwa tena na washtakiwa wote tisa wamepelekwa rumande, gereza la Bukoba.