У нас вы можете посмотреть бесплатно Kesi ya Lissu Yaharishwa Kufuatia Mjadala wa Kisheria Kuhusu Ushahidi Mpya, Wakili Aeleza или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi kesho Jumanne baada ya Mahakama kukabiliwa na mjadala mzito wa kisheria. Upande wa Jamhuri uliwasilisha notisi ya kuleta ushahidi mpya kupitia kifungu cha 308, lakini upande wa utetezi ukapinga vikali hatua hiyo akidai kuwa haikidhi matakwa ya kisheria. Katika hoja zake, Tundu Lissu alisema kuwa notisi hiyo haimtaji shahidi mpya kama sheria inavyotaka, bali inalenga kuongeza ushahidi wa shahidi aliyekwisha kutoa ushahidi wake wakati wa hatua ya awali. Aidha, Lissu alihoji uhalali wa kuingiza masuala ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa wakati huo alikuwa mahabusu, na kuonya kwamba kuruhusu notisi hiyo kutafungua "sanduku la Pandora" la kisheria. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama imeahirisha usikilizwaji hadi kesho kwa ajili ya uamuzi. Unaweza kutufuatilia kupitia; TWITTER: / thechanzo INSTAGRAM: / thechanzo FACEBOOK: / thechanzo TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_... Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105 The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.