У нас вы можете посмотреть бесплатно UGONJWA WA TETEKUWANGA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Katika video hii inazungumza kuhusu sababu, dalili, matibabu, namna ya kuzuia, matarajio baada ya matibabu ya UGONJWA WA TETEKUWANGA, endelea angalia mpaka mwisho kujifunza Tetekuwanga (Chicken pox) ni maambukizi ya virusi yanayosababisha mtu kupata malengelenge yanayowasha mwili mzima. Tetekuwanga ulikuwa ugonjwa uliowapata watoto wengi sana kabla ya kugunduliwa kwa chanjo Kwa watoto,tetekuwanga inasababishwa na virusi wanaoitwa Varicella-zoster. Aina hii ya virusi inasababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes zoster) kwa watu wazima. Ugonjwa wa tetekuwanga unasambaa kwa urahisi zaidi, kwa kugusa au kushika majimaji yanayotoka kwenye malengelenge ya mtu mwenye ugonjwa huu au kama mtu mwenye tetekuwanga atakohoa au kupiga chafya karibu yako. Watu wenye dalili hata za kadri wanaweza kuambukiza wengine. Ukiwa na ugonjwa huu unaweza kuambukiza watu wengine siku ya 1 au 2 kabla ya malengelenge kuonekana – hii inamaanisha unaanza kuambukiza watu, kabla ya kujua kwamba umeambukizwa – na mgonjwa wa tetekuwanga anaweza kuendelea kuambukiza watu wengine mpaka malengelenge yote yanapokauka Visa vingi vya tetekuwanga vinawapata watoto wenye umri chini ya miaka 10. Ugonjwa unakuwa sio mkali sana – ila kuna baadhi wanapata matatizo makubwa. Watoto wakubwa na watu wazima wanapata ugonjwa mkali zaidi kuliko watoto wadogo. Je, nini dalili za tetekuwanga? • Watoto wengi wenye tetekuwanga wanapata homa, maumivu ya kichwa, kupoteza hamu ya kula na uchovu kabla ya upele kutokea. • Upele wa tetekuwanga unatokea siku 10 hadi 21 kuambukizwa. Mtoto anatokewa na vima-lengelenge vidogo kati ya 250 mpaka 500 vinavyowasha, vinavyozungukwa na madoa mekundu kwenye ngozi. • Kwa kawaida Malengelenge yanatokea usoni, kifuani, mgongoni, kichwani na kisha mwili mzima unaanza kuwasha • Baada ya siku moja au mbili, malengelenge yanaanza kuwa na weupe na kisha kutengeneza kigaga. Malengelenge mapya yanatokea kwa makundi - kwenye kope za macho, mdomo na uke. • Baadae yanapona - huwa hakuna makovu yanayotengenezeka, isipokuwa kama mgonjwa alipata maambukizi ya bakteria baada ya kujikuna. Nani yuko kwenye hatari zaidi? Kwa sababu tetekuwanga ni ugonjwa wa kuambukiza, mtu yeyote aliye karibu na mgonjwa yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Utambuzi Ukiambukizwa – daktari anaweza kugundua kuwa una tetekuwanga kwa kuangalia upele na kuuliza maswali kadhaa kuhusu historia yako. Vi- malengelenge vidogo kwenye kichwa mara nyingi vinathibitisha utambuzi huu. Wakati gani utafute matibabu ya haraka? Ni vizuri kufika kwenye kituo cha afya kama unadhani mwanao ana tetekuwanga au kama mwanao ana zaidi ya miezi 12 na bado hajapata chanjo dhidi ya tetekuwanga Uchaguzi wa matibabu ukiwa na tetekuwanga Kwa sababu ugonjwa tetekuwanga unasababishwa na virusi, hatuna tiba kamili ya kuuponyesha. Matibabu ya mara nyingi yanafanyika ili kumpunguzia mgonjwa taabu na shida zinazoletwa na ugonjwa huu, huku tukisubiri mwili upone wenyewe. • Inashauriwa kuepuka kujikuna au kujisugua maeneo yanayowasha. • Hakikisha kucha zako ni fupi ili kuepuka kujichubua ngozi unapojikuna • Vaa nguo nyepesi zisizobana na epuka kuvaa nguo nzito zinazokwaruza katika maeneo yanayowasha - itasababisha ujikune zaidi. • Oga kwa kutumia maji ya vuguvugu na sabuni na kisha jisuuze vyema baada ya kuoga. • Mafuta ya majimaji (moisturizer) yanasaidia kulainisha na kupunguza ukavu wa ngozi. • Epuka kukaa kwenye joto kali na maeneo yenye unyevu mwingi • Dawa aina ya Antihistamine kama vile diphenhydramine zinatumika kupunguza muwasho - lakini kumbuka zinaweza kukusababishia usingizi. • cream ya hydrocortisone pia inatumika sana kupunguza muwasho kwenye maeneo yanayowashwa • Vaa glavu au soksi mikononi ili kupunguza maambukizi yanayotokana na kujikuna hasa usiku unapokuwa umelala usingizini • Watoto wenye tetekuwanga hawapaswi kwenda shule au kucheza na wengine mpaka malengelenge yatakapokauka kabisa. Watu wazima pia hawaruhusiwi kurudi kazini mpaka malenglenge yatakapokauka. Nini cha kutarajia ukiwa na tetekuwanga? • Katiaka hali ya kawaida, mgonjwa anapona bila matatizo yoyote. • Baada ya kupata tetekuwanga, virusi wanabakia mwilini maisha yako yote. mtu1 kati ya watu wazima 10 wanapata mkanda wa jeshi kwa sababu ya virusi hivi kinga mwili inapopungua – mfano wakati wa msongo, ujauzito, uzee au ugonjwa wa ukimwi Emmanuel Mniko #mniko #wikielimu @wikielimu