У нас вы можете посмотреть бесплатно Habari njema kwa Diaspora wakati wa Futari ya Mh. Balozi wa Tanzania UAE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tarehe 14 Machi, 2025 Mhe. Lut. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohammed, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu aliandaa Futari Maalum kwa Watanzania ambao ni Viongozi na Wamiliki wa Makampuni mbalimbali nchini Umoja wa Falme za Kiarabu. Lengo la hafla hiyo, ni kujumuika pamoja na Watanzania hao ili kubadilishana mawazo katika majukumu yao na namna bora ya kushirikiana na Ubalozi katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa manufaa yao na Taifa la Tanzania kwa ujumla. Hivyo, Viongozi na Wamiliki wa Makampuni hao walipata fursa ya kuishauri Serikali yao pamoja na kuonesha utayari katika kushirikiana na Serikali yao kwenye kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Mhe. Lut. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohammed, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini UAE alipata fursa ya kuwafahamisha kuwa Serikali inatambua mchango na umuhimu wa Diaspora katika kuleta maendeleo nchini, hivyo hatua za makusudi zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha Diaspora wanawekewa mazingira wezeshi ya kumtambua kisera na kisheria. Utambuzi huo umezingatiwa kwenye rasimu ya Sera ya Mambo ya Nje ambayo iko katika hatua za mwisho. Mheshimiwa Balozi aliendelea na kusema kuwa katika sera mpya ya Mambo ya Nje ambayo itakuwa na kipengele maalumu cha Diaspora ambapo Serikali imeanza na mkakati wa kuwawekea Hadhi Maalum Watanzania waishio nje ya nchi. Katika hadhi hiyo maalum, Diaspora watakuwa na upendeleo maalumu ikiwa ni pamoja na kuweza kurudi Tanzania kirahisi na kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kichumi tofauti na wageni. Kwa ujumla, Viongozi hao na Wamiliki wa makampuni nchini UAE walishukuru na kuupongeza Ubalozi kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha pamoja. Aidha, wameahidi kushirikiana na Serikali hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali yao inawaandalia mazingira mazuri Watanzania waishio nje kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla. @onlinetv_dailytimes @Wasafi_Media @CrownMediaTZ @kitengetv @CLOUDSMEDIA Maudhui kwa kushirikiana na @onlinetv_dailytimes