У нас вы можете посмотреть бесплатно Waziri Mkuu akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi Chongoleani mkoani Tanga или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu (Februari 16, 2026) amekagua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani mkoani Tanga na amesema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wake. Amesema kuwa mradi huo ni wa kimkakati ambao utagharimu Dola za Marekani bilioni 5.65 ni kielelezo cha undugu kati ya Tanzania na Uganda. “Ninatambua msisitizo uliowekwa na viongozi wetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Miseveni katika utekelezaji wa mradi huu.” Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ambaye yuko mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka uzito unaostahili katika kutekeleza mradi huo ambao umefikia asilimia 81 ya utekelezaji kwa heshima ya undugu kati ya Tanzania na Uganda. “Lakini tutaendelea kuweka uzito unaostahili kwa heshima ya kulinda uhuru wetu kwa kuwa ni nchi huru ambayo inaweza kujitegemea kutekeleza mradi wa kiwango hiki, hiki ni kielelezo kwamba nchi yetu inaweza kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mikubwa ya maendeleo.” Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewatahadharisha watu wanaoanzisha makampuni na kuyaita ya wazawa huku yakiwa yanamilikiwa na wageni ili kunufaika na fursa ya ‘Local Content’ ya Ushirikishwaji wa Watanzania mradi kwamba watakaogundulika watafungiwa na hawatafanya kazi tena nchini. “Wapo wasio waaminifu wanawatumia Watanzania kuanzisha makampuni wanasema ni ya wazawa. Tunataka kuinua kampuni za Watanzania, upo mchezo mgeni anatumia anuani ya Mtanzania ambaye si mnufaika, wale watakaogundulika wanafanya ujanja tutawafungia na hawatafanya kazi tena kwetu.” Waziri Mkuu amesisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuwatapeli Watanzania na kuwaibia fursa. “Tumekupa mradi una nafasi yako tena asilimia kubwa, tunataka hiyo sehemu ndogo inawanufaishe Watanzania na ninyi mnawaibia, wale tuliowapa kazi ya kufuatilia hili tukigundua upo huu mchezo tutakuchukulia hatua kwa kuwa tutajua na wewe ni sehemu yao.” Amesema Mheshimiwa Dkt. Nchemba #chongoleani #tanga_tanzania #bomba_la_mafuta_tanga