У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WA MAKUNGU SASA WAPATA KITUO KIPYA CHA AFYA, MBUNGE ATOA KAULI HIZI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Na Herieth Molla, Iringa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile, amezindua rasmi Kituo cha Makungu chenye thamani ya Shilingi milioni 500, mradi unaotarajiwa kuboresha huduma za afya kwa wakazi zaidi ya 17,000 wa kata hiyo na maeneo ya jirani. Uzinduzi huo unatajwa kuwa sehemu ya mafanikio ya utekelezaji wa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika siku 100 tangu kuchaguliwa na wananchi, hususani katika sekta ya afya ambapo Serikali imeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi. Awali wananchi wa Makungu walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu, hali iliyowaathiri zaidi akina mama wajawazito pamoja na wagonjwa wa dharura, hivyo kukamilika kwa kituo hicho kunatarajiwa kupunguza changamoto hizo na kuokoa muda pamoja na gharama za usafiri. Akizungumza leo wakati wa ziara yake ya siku nne jimboni humo, Mbunge Kihenzile ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, amesema kituo hicho kimejengwa kufuatia maombi maalum yaliyowasilishwa Serikalini kutokana na changamoto za kijiografia na athari za msimu wa mvua katika eneo la Makungu na Mgololo. Amesema wakati wa mvua, baadhi ya maeneo hukatika mawasiliano na kusababisha wananchi kushindwa kufikia huduma muhimu za afya kwa wakati, hali iliyokuwa ikiweka maisha ya watu hatarini. Aidha, mbunge huyo, amemshukuru, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ombi la kujengwa kituo hicho Cha afya Makungu kwani kitakuwa msaada kubwa na kwa wakazi wa Idete pamoja na Kiohela. Mradi huo unatajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha miundombinu ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na kuchochea maendeleo ya kijamii katika ukanda huo.