У нас вы можете посмотреть бесплатно ACT Wazalendo, CUF, NCCR na CHAUMA Watoa Kauli Baada ya Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Dodoma: Vyama vya siasa 18 vyenye usajili wa kudumu kati ya vyama 19 vimeshiriki katika kikao cha kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais wabunge na madiwani, unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025, huku chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikiwa hakina muwakilishi. Vyama viilivyo shiriki kwenye utiaji saini ni Chama cha Mapinduzi CCM, ACT wazalendo, Chama cha Wananchi CUF, Chama cha kijamii CCK, ADC, DP, Demikrasia Makini, NCCR Mageuzi , NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, ADA TADEA, AAFP, CHAUMA, UMD na UPDP. Chama cha ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi, Chama cha Wananchi CUF na Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA, ni miongoni mwa vyama vilivyo zungumza vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa zoezi hilo, huku vikionesha kuridhishwa na mchakato wa zoezi hilo Kifungu cha 162 kidogo cha pili cha Sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani Sheria namba moja [1], kinaweka sharti la ulazima kwamba kila chama cha siasa, kila mgombea kabla hajawasilisha fomu ya uteuzi wanapaswa kusaini na kuzingatia Kanuni za maadili ya uchaguzi wakati wote wa kampeni za uchaguzi na utaratibu wa utekelezaji wake. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 162 cha Sheria ya uchaguzi wa uraisi, wabunge na madiwani Sheria namba moja [1] ya mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliandaa rasimu ya kanuni za maadili za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani za mwaka 2025. Baada ya kukamilisha maandalizi ya rasimu ya kanuni hizo tume iliziwasilisha kwa vyama vya siasa kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni yao kuanzia Machi 1, 2025 hadi Machi 14, 2025. Maoni hayo yalijumuishwa katika Kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani za mwaka 2025. Hata hivyo, maoni ya kukamilisha rasimu ya Kanuni za maadili ya uchaguzi wabunge, Rais na madiwani za mwaka 2025 yalirejeshwa tena kwa vyama vya saisa Aprili 4, 2025 na hivyo kualikwa kwa ajili ya utiaji saini Aprili 12, 2025. Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema, hadi leo Aprili 12, 2025 hawajapokea maoni tofauti ya rasimu, hivyo imechukuliwa kwamba rasimu hii imekubaliwa na pande zote tatu kwa maana ya vyama vya siasa, Serikali naTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Imeandaliwa na Jackline Kuwanda Unaweza kutufuatilia kupitia; TWITTER: / thechanzo INSTAGRAM: / thechanzo FACEBOOK: / thechanzo TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_... Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105 The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.