У нас вы можете посмотреть бесплатно KITUO CHA UPANDIKIZAJI MIMBA CHAZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo amezindua huduma tatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo kituo cha upandikizaji mimba, gari la tiba kwa njia ya mkoba pamoja na kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 15 wenye umri chini ya miaka mitano waliozaliwa na tatizo la kutokusikia. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amesema kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia hospitali yake ya Taifa Muhimbili ameanza zoezi la kupandikiza mimba huku akiwataka Watanzania kuchangamkia fursa hiyo. Dkt. Mpango amesema hayo leo Septemba 11, 2024 baada ya kuzindia kitua cha upandikizaji mimba (IVF) cha Dkt. Samia Suluhu Hassan, gari la huduma tembezi za Afya (Mobile Medical Services) pamoja na kuwasha vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. "Ninawasihi Watanzania wenzangu sasa tuchangamkie fursa zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, huduma ambazo ni bora na zenye gharama nafuu ikiwemo huduma za kibingwa za upandikizaji mimba." Amesema Dkt. Mpango