У нас вы можете посмотреть бесплатно KILIO KWA RAIS SAMIA, BAADA YA MAMIA KUSHUHUDIA YANAYOENDELEA MASHAMBA YA MIWA BAGAMOYO SUGAR или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Zaidi ya wakulima 290 kutoka chama wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Wilayani Bagamoyo wameiomba Serikali kuwapatia eneo la Hekta 2000 lililipo pembezoni mwa shamba la miwa ya Kiwanda cha Sukari Bagamoyo ili waanzishe kilimo cha miwa na kuuza kiwandani hapo kama wazalishaji wa Nje. Timu ya wakulima na wanachama wa chemba ya biashara,viwanda na kilimo wilaya ya Bagamoyo wakiwa katika shamba la miwa la Bagamoyo sugar kujifunza namna ambavyo wanaweza kuanzisha kilimo cha miwa kwa ajili kuuzia kiwanda cha kuzalishia sukari cha Bagamoyo kama wakulima wa nje, wakulima hao wamesema fursa za kilimo cha miwa zilizopo katika eneo hilo ni kubwa na zinaweza kuwanufaisha wadogo wadogo na hivyo kuimba serikali kuwapatia eneo pembezoni mwa shamba hilo ili kuanzisha kilimo hicho ili kuunga mkono juhudi za serikali kuleta mapinduzi ya kilimo. Mtaalamu wa kilimo katika shamba hilo Bwana Saguti Ibrahim ameelezea uwepo wafursa nyingi kwa wakulima wanaozunguka eneo hilo , na hivyo kazi ni wao kuzichangamkia tu. Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo mkoa wa Pwani Said Mfinanga amesema wanachama hao wamejipanga tayari kuanzisha kilimo hicho lakini wanakwamishwa na upatikanaji wa hati ya eneo hilo ambayo waliomba muda mrefu bila mafanikio.