У нас вы можете посмотреть бесплатно MWENYEKITI UVCCM AJILIPUA "CHONGOLO ,NJOO UGOMBEE UBUNGE" ADAI AKILI YAKE BADO INAPASWA KUTUMIKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#jambotv Njombe Wakati joto la uchaguzi mkuu hapo mwakani likiendelea kushika kasi nchini na kupelekea viongozi mbalimbali kuanza kuonekana wakihitaji nafasi za Ubunge na udiwani huku waliopo madarakani nao wakiwa na hofu kubwa juu ya nafasi zao,baadhi ya viongozi hususani wa Chama cha Mapinduzi pia wameonekana wakiwa majukwaani wakiendelea kuwaunga mkono na kuwapa nguvu wanaCCM wenye nia ya uongozi.Chama cha Mapinduzi nacho kwa nyakati tofauti kimekuwa kikiwaonya viongozi wa Chama hicho kujihusisha na wagombea jambo ambalo linatajwa kukigawa Chama hicho kutokana na viongozi wengi kuanza kushiriki kampeni za chini huku wakiwa na viongozi wao mfukoni.Jimbo la Makambako lililopo mkoani Njombe ni miongoni mwa majimbo yanayoonkana yakitikiswa katika mkoa huo kutokana na taarifa za aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Daniel Chongolo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Songwe kwa sasa akihitaji kutia nia kwenye jimbo hilo ili kumng'oa kigogo wa muda mrefu ndugu DEO SANGA (JAH PEOPLE) na akitajwa kuonekana mara kwa mara mkoani Njombe.Erick Ngole ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa hamasa ya uandikishwaji kwenye daftari la mpiga kura pamoja na elimu mbalimbali ikiwemo ya mikopo iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo wilaya na kufanyika katika jimbo la Makambako huku mgeni rasmi akiwa Daniel Chongolo ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa amesema Jumuiya hiyo itaendelea kuwaunga mkuono viongozi wanaokwenda sambamba na jumuiya huku akimuomba Chongolo kugombea nafasi yoyote wilayani Njombe kwa kuwa akili yake inapaswa kutumiwa na watu wa Njombe.