У нас вы можете посмотреть бесплатно ASKOFU MCHAMUNGU AFANYA ZIARA PAROKIA YA BANGULO: AWAPONGEZA WAAMINI KWA HATUA KUBWA YA MAENDELEO. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ASKOFU MCHAMUNGU AFANYA ZIARA PAROKIA YA BANGULO: AWAPONGEZA WAAMINI KWA HATUA KUBWA YA MAENDELEO. Parokia ya Bangulo, DAR ES SALAAM Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Hendry Mchamungu leo January 04, 2026 amefanya ziara ya kichungaji katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Bangulo ikiwa ndio inatimiza mwaka mmoja tangu ianzishwe kwake. Alipokanyaga ardhi ya parokia hiyo kwa mara ya kwanza tangu iwe parokia rasmi mwaka jana January 04, 2025 Askofu Mchamungu alipokelewa na Paroko Fr Titus Ngapemba pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Parokia hiyo na kukabidhiwa shada la Maua. Akiwa parokiani hapo, Askofu Mchamungu aliwapongeza waamini wa parokia hiyo pamoja na Paroko wao kwa maendeleo makubwa tena ya kasi ya kuendeleza parokia yao. Amezindua nyumba ya mapadre, amebariki uwanja ekari 1 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa, amewaimarisha kiroho vijana 117 (Kipaimara) na amemsimika rasmi Paroko na kumkabidhi funguo za parokia hiyo. Nao waamini kupitia Risala yao iliyosomwa mbele yake na Katibu Msaidizi wa Kamati Tendaji ya Parokia Ndg Anthony Valonge wamemshukuru Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu sana Judah Thaddeus Ruwa'ichi-OFMCap kwa kuwapatia hadhi ya Parokia na hivyo wanakusudia kuanza ujenzi wa Kanisa lao baadae mwaka huu.