У нас вы можете посмотреть бесплатно WALIORUHUSU WATALII KUSHUKA KWENYE MAGARI KUTIZAMA NYUMBU WAKIHAMA KIKAANGONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limethibitisha tukio la baadhi ya watalii kushuka kutoka kwenye magari yao katika eneo la Kogatende, kivuko namba nne ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti, kinyume na taratibu na sheria za uhifadhi. Akilizungumzia tukio hilo, Kamishina Msaidizi wa Hifadhi, Kitengo cha Mawasiliano wa TANAPA, Catherine Mbena, amesema tukio hilo lilitokea Julai 21, 2025 ni la kweli kama picha na video zinazosambaa mitandaoni zinavyoonyesha na kuwa tukio hilo ni kinyume na utaratibu wa uhifadhi za Taifa. "Ni kweli tukio hili limetokea ambapo watalii walishuka kwenye magari katika eneo ambalo hairuhusiwi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Hifadhi za Taifa Tanzania," alisema Mbena. Alieleza kuwa askari wa TANAPA waliokuwa katika kikosi cha Kogatende walifika eneo la tukio mara moja na kuwaelekeza watalii hao kurejea ndani ya magari yao na kuwatahadharisha juu ya hatari na madhara ya kitendo hicho. Mbena alifafanua kuwa kushuka kutoka kwenye magari hufanya watalii kuwa hatarini kushambuliwa na wanyama wanaowinda wanyama hao kama simba na chui, kuharibu mfumo mzima wa msafara wa Nyumbu, pamoja na kuharibu mazingira ya hifadhi. "Tayari tumeshayabaini magari yote yaliyohusika na hatua kali zimeanza kuchukuliwa dhidi ya waongozaji wa watalii hao," alisema Mbena. TANAPA imetoa wito kwa wadau wote wa utalii kuendelea kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za hifadhi ili kulinda wanyamapori na kuhakikisha usalama wa wageni.