У нас вы можете посмотреть бесплатно HAKUNA KUONGEZEANA MUDA: WAZIRI AWESO AELEKEZA MRADI WA MAJI MPANDA UKAMILIKE KWA HARAKA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Maji, Mhe. Juma Hamidu Aweso (Mb), ameagiza Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa. Ameyasema hayo leo Julai 24, 2025 alipotembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Ameeleza kuwa hakuna sababu ya kuongezewa muda kwa Mkandarasi kwa kuwa Serikali imeshatoa fedha zote za utekelezaji wa mradi, hivyo kazi inapaswa kufanyika kwa ufanisi mkubwa, mchana na usiku, hadi kukamilika kwake. Ameongeza kuwa mkazo mkubwa unatakiwa kuwekwa katika ujenzi wa dakio, ikiwa ni sehemu muhimu ya miundombinu ya mradi huo, kwa lengo la kufanikisha dhamira ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani na kuboresha maisha ya wananchi. Katika hatua nyingine, Waziri Aweso ametumia ziara hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha shilingi bilioni 22 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya fedha za maendeleo zinazolenga kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amesema kuwa Serikali tayari imetumia zaidi ya shilingi bilioni 65 katika kuboresha sekta ya maji mkoani humo, hatua iliyochangia kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa maji kwa wananchi. Amefafanua kuwa kabla ya juhudi hizo, hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa chini ya asilimia 60, lakini kwa sasa imefikia asilimia 68.5 mijini na asilimia 77.3 vijijini, ikiwa ni mafanikio ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita.