У нас вы можете посмотреть бесплатно KAMISHNA wa POLISI Atinga UNGUJA KUZUNGUMZA na WANAKIJIJI... или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KAMISHNA wa POLISI Atinga UNGUJA KUZUNGUMZA na WANAKIJIJI... Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii wa Jeshi la Polisi Dkt. Mussa Ali Mussa amewataka watendaji wa Shehia kwa Visiwani Unguja na Watendaji Kata kwa Tanzania Bara kuwatumia Askari Kata au Shehia kuwa makatibu wa kamati zao za Ulinzi na Usalama za Shehia au Kata kwa kuwa askari hao ni wataalamu wa mambo ya Ulinzi na Usalama na watakua ni msaada mkubwa katika kutatua kero mbalimbali katika maeneo yao. Dkt Mussa amesema pamoja na maeneo mengi Tanzania bara na Visiwani kuitikia wito wa Ushirikishwaji wa Jamii kwa dhana ya kuunda vikundi vya Ulinzi shirikishi, amesema dhana hiyo ni nzuri sana ingawa wanapaswa pia kuwatumia askari kata au shehia waliopelekwa kwenye maeneo yao ili kutatua kero zingine za wananchi ambazo haziwezi kutatuliwa kwa kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi bali kwa kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi kwa kumtumia askari huyo. Kamishna Mussa amesema bila kuwa na mfumo mzuri wa kiulinzi, maendeleo ya Kiuchumi kama ya kujipatia kipato na maendeleo ya Kijamii kama kuwa na shule na hospitali havitaimarika na kusisitiza kuwa mfumo huo unatakiwa kuanzia ngazi za chini kabisa kwa kutumia Kamati za Ulinzi na Usalama za Kata au Shehia ambazo mwenyekiti wake ni Shekha au Mtendaji Kata na Katibu wake awe Polisi Kata au Shehia. Dkt Mussa amesema hayo akiwa katika ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa askari kata au shehia na ameongeza kuwa kwa tathmini aliyoifanya tangu ameaza ziara yake katika mikoa mitatu ya Tanzania Bara ambayo ni Morogoro, Tanga na Pwani na Sasa Mkoa wa Kaskazini Unguja Visiwani Zanzibar, tathmini imeonesha kuwa Maeneo yote hayo Amani na Usalama upo ila utulivu umepungua kwa kiasi kikubwa. Amesema Kukosekana kwa utulivu kunatokana na kero ndogondogo zinazojitokeza katika jamii ambazo amesema zikifumbiwa macho ndiyo zinatengeneza uhalifu mkubwa na kusababisha Polisi kutumia nguvu kubwa na kupambana na uhalifu badala ya kuzuia uhalifu na sababu hii ndiyo imepelekea Jeshi la Polisi kuanzisha utaratibu wa kupeleke askari mmoja katika kila kata au shehia akasaidiane na mtendaji kata au sheha kutatua kero zinazojitokeza katika maeneo yao. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvo... ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506) ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2 ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline