У нас вы можете посмотреть бесплатно 🔴 KAMATI YA SIASA SONGEA MJINI YATEMBELEA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU, WAMPONGEZA, WAWASHUKURU WADUA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea Mjini, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Msolomi, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa CCM Songea Mjini. Ziara hiyo imefanyika katika mtaa wa Mshangano, Manispaa ya Songea, ambako nyumba hiyo ya Katibu wa CCM Songea Mjini inaendelea kujengwa. Kamati hiyo imeelezwa hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi huo pamoja na mipango iliyopo hadi kukamilika kwake. Baada ya kukagua mradi huo, wajumbe wa Kamati ya Siasa wamepongeza juhudi zinazofanywa na Katibu wa CCM Songea Mjini katika kusimamia ujenzi wa nyumba hiyo, wakieleza kuwa mradi huo ni muhimu katika kuimarisha mazingira ya kazi na makazi ya viongozi wa chama. Kwa upande wake, Katibu wa CCM Songea Mjini, Ndugu James Mgego, ameishukuru Kamati ya Siasa kwa ziara yao pamoja na ushauri walioutoa. Aidha, amewashukuru wadau mbalimbali walioweza kujitokeza kuchangia kwa hali na mali kufanikisha ujenzi wa nyumba hiyo. Ndugu Mgego ametoa wito kwa wadau wengine na wanachama wa CCM kuendelea kushirikiana na chama katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisisitiza kuwa mshikamano na ushirikiano ndio nguzo kuu ya mafanikio ya chama na maendeleo ya jamii kwa ujumla.