У нас вы можете посмотреть бесплатно KUSOMESHA RUBANI MOJA MILIONI 200 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali ya Awamu ya Sita ina miradi mikubwa ya kimkakati, Chuo hiki ni moja ya vyuo vichache nchini vilivyopewa jukumu la kuandaa rasilimali watu ambapo kinaendesha Vituo viwili vikubwa vya Umahiri. Serikali imekopa takriban Shilingi bilioni 49 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Taaluma za Usafiri wa Anga na Operesheni za Usafirishaji ambacho kina majukumu ya kutayarisha Wataalam wa Sekta ya Usafiri wa Anga. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof Zacharia Mganilwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho sambamba na vipau mbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Prof Zacharia amesema kuwa Fedha hizo zimegawanywa katika upande wa ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kufundishia Wataalam ambapo jumla ya majengo matano yatajengwa Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi bilioni 21 na baadae kujengwa majengo mkoani Kilimanjaro ili kutoa Nafasi kwa wazawa kupata nafasi ya kufundishwa hapa nchini kupitia ndani ya Viwanja vya Ndege. Aidha prof Zacharia ameongeza kuwa Fedha nyingine zitatumika kununua vifaa vya mafunzo, kwa kuwa Kituo kitafundisha Marubani, Wahandisi wa Ndege, Wahudumu Ndani ya Ndege na Waajiriwa wa Viwanja vya Ndege, chuo kimenunua ndege mbili zenye injini moja za mafunzo ambazo ziko njiani kuja Tanzania kwa gharama ya Shilingi Dola za Marekani milioni 1.2. Katika hatua nyingine amesema kuwa Mwaka wa Fedha, 2022/23, Chuo kitanunua tena ndege yenye injini mbili kwa ajili ya mwanafunzi kukamilisha mafunzo yake kwa sababu mafunzo ya Urubani yanamtaka mwanafunzi ajifunze ndege yenye injini moja na injini mbili. Sanjari na hayo prof Zacharia amesema kuwa Kumfundisha Rubani mmoja nje ya nchi ni Shilingi milioni 200, "hivyo Serikali inapofanya uwekezaji huu inalifanya Shirika la Ndege Nchini kuleta matumaini ya nchi katika kukuza utalii na uchumi kwa sababu Wataalam wa usafiri wa anga watafundishwa hapa hapa nchini". Katika hatua nyingineTanzania ina zaidi ya ndege 400 zilizosajiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambapo asilimia 60 ya Marubani ni wageni, hivyo ndege hizi zitakapofika vijana wa kitanzania wenye sifa za kusomea Urubani watafundishwa na kupata ajira ndani ya nchi. "Kwa mara ya kwanza tangu tumepata Uhuru, chuo kinafundisha pia Diploma ya Uchomeleaji na Uungaji wa Bomba la Mafuta, hii itasaidia tusipeleke tu madereva na kina mama lishe bali tupeleke pia Wataalam watakaokuwa wanachoma bomba la mafuta". alisema prof Zacharia #Tuna Kituo kingine cha Umahiri cha Kikanda katika usalama Barabarani ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Dola za Marekani Milioni 2.1 kwa mradi wote kikiwa na majukumu ya kufanya utafiti wa sababu za ajali na nini kifanyike pamoja na kufundisha Wakufunzi wa Madereva katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. #rsmmediaNewsUpdates #youtubersmmedia