У нас вы можете посмотреть бесплатно BANDARI YA MBAMBA BAY KUINUA UCHUMI WA KUSINI NCHI ZA TANZANIA,MALAWI NA MSUMBIJI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema serikali inatambua umuhimu mkubwa wa mradi wa ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay iliyopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, akibainisha kuwa mradi huo ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na nchi za jirani za Malawi na Msumbiji. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Prof. Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 80 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka 2026. Ameeleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 47, hatua inayoonesha kasi nzuri ya ujenzi. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amesema uwekezaji katika mradi wa bandari ya Mbamba Bay unaufanya mkoa wa Ruvuma kuwa mkoa wa kimkakati kibiashara. Amesisitiza kuwa bandari hiyo itakuwa kichocheo muhimu cha biashara za kikanda zitakazohusisha nchi jirani ikiwemo Malawi na Msumbiji. Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mheshimiwa John Nchimbi, ameiomba Wizara ya Uchukuzi kuingilia kati changamoto ya usafirishaji wa makaa ya mawe katika mwambao wa Ziwa Nyasa. Amesema bado kuna mvutano kati ya Mamlaka ya Bandari na wafanyabiashara wa makaa ya mawe, hali inayokwamisha shughuli za kibiashara na ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.