У нас вы можете посмотреть бесплатно Watumishi wahimizwa kufanya mazoezi kwa faida za afya zao или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ladislaus Lwoga, Mkufunzi wa michezo kutoka Idara ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo amewahimiza watumishi wa umma juu ya kufanya mazoezi muda wote badala ya kusubiri kuanza kufanya mazoezi kunapotokea mashindano au tukio fulani. Ametoa wito huo, Desemba 06, 2025 wakati akizungumzia ushiriki wa SUA katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA 2025) yaliyofanyika mkoani Morogoro, ambapo amesema Chuo kilitoa jumla ya watumishi 36 kushiriki mashindano hayo ambapo imefanikiwa kuibuka mshindi katika mchezo wa kukimbia na gunia. Amesema kutamatika kwa mashindano ya SHIMMUTA 2025 kusiwe mwisho wa mazoezi kwani mazoezi yanatakiwa kuwa sehemu ya maisha ili uweze kujenga mwili, afya na kujenga ujamaa (socialization) na wenzako. "Ofisi yetu ya michezo iko wazi muda wote, tuna vifaa ambavyo mtumishi anaweza kuvitumia muda wote - tunatambua umuhimu wa mazoezi katika kujenga mwili na kuongeza ari ya kufanya kazi", alisema Lwoga. Mashindano ya SHIMMUTA hufanyika kila mwaka yakihusisha watumishi kutoka Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania.