У нас вы можете посмотреть бесплатно MAUMIVU YA MISULI NA VIUNGO: Kujitibu mwenyewe nyumbani или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
https://wikielimu.org/ #wikielimu #DRMNIKO Maumivu ya misuli na viungo bila uvimbe wowote au wekundu wowote, yanaweza kusababishwa na makazo wa misuli, maambukizi ya virusi au kama umefanya kazi ngumu. Mara nyingine utakuta sababu yaw ewe kuwa na maumivu ya misuli au viungo haifahamiki. Mara nyingi maumivu ya aina hii huwa si kitu cha kukutia wasiwasi. Maumivu ya misuli na viungo ya aina hii, mara nyingi huisha tu yenyewe baada ya muda. Ni kweli kwamba yapo magonjwa au matatizo ambayo yanaweza kusababisha maumivu ya misuli na viungo kama; magonjwa ya tezi dundumio (thyroid diseases), kansa, kuvimba kwa misuli (polymyositis) au maumivu ya shingo, mabega na nyong akwa wazee kunakoitwa polymyalgia kitaalamu. Tatizo kama fibromyalgia linasababisha maumivu ya misuli, uchovu mwingi na kushindwa kupata kulala vizuri. Mtu mwenye hili tatizo pia anaweza kuwa na matatizo ya tumbo, viungo vinakakamaa sana asubuhi, hofu kupita kiasi, kupteza kumbukumbu na dalili nyingine nyingi. Kwa hiyo, kama una maumivu ya misuli na viungu na una homa, umepungua uzito au unajihisi uchovu mkubwa sana, nenda kamwone daktari ili atambue tatizo lako. Ila kama sivyo, jaribu kufanya mambo yafuatayo ukiwa nyumbani kwa wiki kadhaa uone kama yatasaidia. Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama una maumivu ya viungo na misuli Pumzika na fanya mazoezi, hakikisha unapata usingizi wa kutosha ili kupumziksha mwili. Unaweza kutembea, kuendesha baiskeli au kuogelea ili kuweka sawa mwili. Oga maji ya moto, pata massage na fanya mazoezi ya kujinyoosha mara kwa mara. Kama unafanya kazi katika mazingira yasiyo rafiki yabadilishe. Kama unasimama muda mrefu kazini, vaa viatu vyenye “sponge sole”. Badilisha kiti unachokaa kama unafanya kazi ukiwa umekaa. Kama maumivu yanapungua wakati wa likizo au weekend, msongo wa mawazo kazini unaweza kuwa sababu ya mwili wako kuuma. Dawa za maumivu kama acetaminophen, asprin, ibuprofen, naproxen au ketoprofen zinaweza kukukafaa. Ni vizuri kuongea na daktari kama umetumia dawa hizi kwa wiki tatu na haupati nafuu yoyote. Kama umeumia; anza kwa kuweka kitu cha baridi kama barafu iliyofunikwa kwenye kitambaa ili kupunguza eneo hilo kuvimba kwa masaa 24 ya mwanzo. Baada ya masaa 24 unaweza kuanza kuweka vitu vya moto, kama maji ya mto yaliyowekwa kwenye chupa. Iweke kwenye maeneo yanayouma, itasaidia kufungua mishipa ya damu, ili damu ufike kwa urahisi kwenye eneo lililoumia kwa uponyaji zaidi. Kwa wazee; Kwa wale wenye tatizo la fibromyalgia tulilozungumza hapo nyuma – mazoezi ndio mpango mzima wa matibabu. Fanya mazoezi mepesi ambayo hayasulubu viungu, mazoezi kama kutembea, kuogelea au kuendesha baiskeli; usifanye mazoezi kama kukimbia au kucheza tennis. Ukianza mazoezi, maumivu yataongezeka kwa muda, ila baada ya muda yatapungua kabisa. Jikaze na uvumilie. Kama umefanya yote ndani ya wiki mbili nab ado hujisikii vizuri, hakikisha unaenda kuonana na daktari