У нас вы можете посмотреть бесплатно DK NCHIMBI AISHANGAA KIGOMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ameonekana kuishangaa Kigoma ilivyopiga hatua za maendeleo tofauti na miaka 25 iliyopita. Ameonesha mshangao hao alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara mjini Kigoma Agosti 4, 2024 Dk Nchimbi yupo kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, na baada ya hapo ataendelea na ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Geita, Kagera, Mwanza na Mara. Akihutubia katika mkutano huo, Dk Nchimbi aliimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuufungua mkoa huo kimaendeleo ambapo kwa miaka mitatu ameupatia zaidi ya sh. Trilioni 11.4 za maendeleo.ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR, miundombinu ya barabara, maji, elimu na umeme. Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu. Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.