У нас вы можете посмотреть бесплатно CCM YAMKATAA NAPE KISA KAULI YA USHINDI "NJE YA BOKSI" MWENYEWE ATOA UFAFANUZI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana iliyotafsiriwa na watu wengi. “Nimeona mjadala wa video hii. inapotoshwa kwa kukata vipande watakavyo wapotoshaji. Msingi wa mjadala huu ulikuwa utani wa hoja ya zamani ya “goli la mkono”.. uliorushwa wakati naongea ndio maana kuna kicheko kabla. Haikuwa serious version. Mimi muumini wa uchaguzi huru na haki. Vizuri tuendelee kushindana kwa hoja,”ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X leo Jumanne Julai 16, 2024. Nape ameibuka kuelezea hoja hiyo ikiwa ni saa chache tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla leo, aseme kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho. “Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” amesema. Nnauye aliyewahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, alitoa kauli hiyo jana Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi. Muktadha wa kauli hiyo ilikuwa ni kuwahakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Nnauye ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alitoa kauli hiyo. “Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi tu mkishamaliza unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea,” alisema.