У нас вы можете посмотреть бесплатно NDEGE KUTOKA NJE KUTUA ARUSHA AIRPORT или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kiwanja cha ndege cha Arusha, kimepata kibali cha kutua ndege ndogo zinazotoka nje ya Tanzania, baada ya miaka mingi kutumika kama kiwanja cha ndani. Awali ndege zote zinazobeba abiria wanaotoka nje kwenda Arusha na wanaotoka Arusha kwenda nje ya nchi wakiwemo Watalii, walilazimika kutumia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kwa ajili ya ukaguzi wa nyaraka za kusafiria na mizigo. Kwa sasa Kiwanja cha Arusha kimetimiza matakwa yote ya kikanuni na kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji, Maafisa Forodha, nk. Kampuni ya ndege ya Flightlink, imekuwa ya kwanza kufanya safari ya moja kwa moja kutoka Kiwanja cha ndege cha Arusha kwenda Nairobi, Kenya na kurudi Arusha. Jumatatu Juni 16, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshuhudia ndege hiyo ikitua katika kiwanja hicho ikitokea moja kwa moja Nairobi, na baadaye kuzungumza na Wana Habari.