У нас вы можете посмотреть бесплатно PSSSF YATOA MSAADA WA VIFAA SAIDIZI KWA JUMUIYA YA WATU WENYE ULEMAVU WA MACHO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma PSSSF leo 6 februari 2026 wametoa msaada wa vifaa saidizi vyenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa Jumuiya ya wasioona Tanzania (TAB). Vifaa hivyo ni pamoja na mashine 3 za kuandika nukta nundu pamoja na fimbo nyeupe 346 zinazokunjika mara tano, na fimbo nyeupe 106 zinazokunjika mara sita. Vifaa hivyo vitawasaidia wasioona kusoma na kuandika, pamoja na kutembea sehemu mbalimbali kwa usalama zaidi. Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa PSSF kanda ya Ilala amesema kuwa ni kawaida kwa PSSSF kurudisha msaada kwa jamii wakiunga mkono kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani "Kazi na utu" Nae mratibu wa idara ya vijana Jumuiya ya wasioona Bw. Bakari Hasan Shemaeze maarufu kama Mr High ameishukuru PSSSF kwa msaada huo huku akieleza kuwa licha ya kuomba msaada sehemu mbalimbali lakini PSSSF limekuwa shirika la kwanza kujibu maombi yao na kuwapatia msaada waliouhitaji. Aidha mkurugenzi mkuu wa PSSSF ameahidi kuwajengea choo katika ofisi ya Jumuiya ya wasioona Tanzania hitaji waliloliomba wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo. Pata habari motomoto za muziki, burudani, utamaduni, siasa, matukio, habari za kina, na michezo kupitia Wasafi Media. Hii Ni Yetu Sote. https://wasafimedia.co.tz/ 𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2025 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅. #wasafi #wasafitv #wasafifm