У нас вы можете посмотреть бесплатно BALAA JIPYA, ZANZIBAR ITAKUA KAMA ULAYA, NYUMBA ZA KWA MJERU - KIKWAJUNI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Katika jitihada za kuimarisha na kukuza hadhi pamoja na muonekano wa Mji Mkongwe, Stone Town Conservation and Development Authority imefanya kikao maalum na kampuni ya Infinity Development kwa lengo la kujadili mradi wa ujenzi wa nyumba za makaazi katika eneo la Kikwajuni (Kwa Mjeru). Kikao hicho kimefanyika Machi 5, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mamlaka ya Mji Mkongwe, Mkoa wa Mjini Unguja, na kuwahusisha wadau pamoja na wataalamu mbalimbali wa sekta ya ujenzi na mipango miji. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi na Mipango ya Mji Mkongwe, Mhandisi Yasser DeCosta amesema lengo la kikao hicho ni kuwapa fursa wawekezaji wa Infinity Development kuwasilisha michoro ya mradi waliyoibuni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makaazi katika eneo la Kikwajuni. Amesema uwekezaji huo una umuhimu mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani unatoa nafasi kwa wadau na wataalamu kutoa maoni yao kuhusu utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuangalia namna bora ya kupanga maendeleo ndani ya Mji Mkongwe. Aidha, Mhandisi DeCosta amesisitiza kuwa pamoja na kuanzishwa kwa majengo ya kisasa katika eneo hilo, ni muhimu kuhakikisha kunakuwepo uwiano kati ya majengo mapya na majengo ya kale ya Mji Mkongwe ili kulinda utamaduni, historia na urithi wa eneo hilo. #ASAMOnlineTV #MjiMkongwe #Zanzibar #MaendeleoYaMiji #Uwekezaji