У нас вы можете посмотреть бесплатно DC ARUSHA AZIMA MGOMO WA WAFANYA BIASHARA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DC ARUSHA AZIMA MGOMO WA WAFANYA BIASHARA Arusha. Mgogoro uliokuwa ukitishia kusababisha mgomo wa wafanyabiashara jijini Arusha umefikia tamati, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, kuingilia kati na kutoa maelekezo maalumu kuhusu upangaji wa maeneo ya biashara. Awali, wafanyabiashara wenye maduka walitishia kufunga biashara zao wakilalamikia vitendo vya wamachinga kupanga bidhaa mbele ya maduka yao, hali waliyoeleza kuwa inahatarisha uwekezaji wao, kupunguza mapato na kuathiri biashara zao, licha ya wao kuendelea kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali. Akizungumza kufuatia malalamiko hayo, DC Mkude alitoa muda wa siku tatu kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanaofanya biashara katika maeneo ya barabara kuondoka mara moja, akisisitiza kuwa wanafanya biashara kinyume cha sheria. Aidha, amewataka wafanyabiashara hao kuhamia kwenye vizimba pamoja na maeneo maalumu yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya shughuli za biashara, ili kudhibiti migongano na kuhakikisha sheria, utaratibu na usalama vinafuatwa. #arusha #machinga #tanzania