У нас вы можете посмотреть бесплатно Ukweli Kuhusu Maisha na Kazi Ughaibuni или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wengi huota kuishi Ulaya — Paris, London, Berlin… lakini wachache sana wanajua uhalisia wa maisha na kazi huko! Katika episode hii ya Soga za Diaspora, tunavunja ukimya na kuzungumza waziwazi kuhusu ukweli wa maisha na kazi Ughaibuni, tuliangalia safari ya Engineer Felician MATINYA, ambaye anaishi na kufanya kazi katika jiji la Paris, Ufaransa. Je, ni rahisi kweli kupata kazi Ulaya? 💼 Je, mishahara inalingana na gharama za maisha? 💶 Na je, maisha ni mazuri kama yanavyoonekana kwenye mitandao ya kijamii? 📸 Tunaangalia: ✨ Fursa halisi za kazi kwa Watanzania na Waafrika Ughaibuni 💪 Changamoto za lugha, kazi, makazi na utamaduni 🧭 Safari za mafanikio na vikwazo vinavyowakumba wengi 💡 Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuhamia Ulaya Hii ni zaidi ya simulizi — ni kioo cha uhalisia wa maisha Ughaibuni, kutoka kwa watu wanaoishi na kufanya kazi huko kila siku. 👉 Tazama hadi mwisho ujifunze kile ambacho hakisemwi mara nyingi: “Ndoto ya Ulaya si hadithi — ni safari yenye ukweli wake.” 💬 Toa maoni yako: Wewe unafikiri nini kuhusu maisha ya kazi Ughaibuni? 🔔 Subscribe kwa vipindi zaidi vya Soga za Diaspora — tunazungumza ukweli, tunagusa maisha. Vitu vilivyoongelewa: 00:00 - Mwanzo 00:00:39 - Safari ya kitaaluma ya Felician Matinya Ufaransa. 00:01:58 - Sababu zilizomvutia Felician kuchagua nchi ya Ufaransa kwa masomo na taaluma yake. 00:02:46 - Changamoto na njia alizopitia Felician kupata kazi yake ya kwanza nchini Ufaransa. 0:08:20 - Je, kuna uwezekano mtu ambaye hajui kabisa Kifaransa kupata kazi nchini Ufaransa? 00:09:56 - Baadhi ya sekta na taaluma sahihi kwa wageni nchini Ufaransa (Hot cake careers for foreigners) 00:12:50 - Umuhimu wa kupitia katika mfumo wa elimu wa Kifaransa ili kufahamu mazingira na tamaduni za kazi. 00:15:32 - Vitu na mazingira ya Kifaransa vinavyofanya Ufaransa kuwa sehemu sahihi kwa Felician Matinya kukuza taaluma yake. 00:18:17 - Mtazamo wa Felician kabla na baada ya kuja Ufaransa 00:20:20 - Namna sahihi ya mwanafunzi kujinadi na kupata kazi yake ya kwanza nchini Ufaransa. 0:22:22 - Sifa na tabia za kitaaluma zinazopewa kipaumbele na waajiri nchini Ufaransa. 00:25:05 - Taboo ambazo hazipaswi kuongelewa wala kujadiliwa maeneo ya kazi. 00:27:48 - Miji sahihi kufanya kazi nchini Ufaransa, hasa wageni. 0:30:13 - Umuhimu wa networking katika kujenga na kukuza taaluma Ufaransa 00:31:40 - Namna co-optation (kupigiana pande) inavyofanya kazi Ufaransa. 00:34:33 - Je, naweza kumpigia pande (co-opt) ndugu yangu kazini? 00:36:05 - Je kuna ubaguzi katika mazingira ya kazi nchini Ufaransa? 00:37:54 - Je kuna upendeleo katika mazingira ya kazi nchini Ufaransa? 00:41:25 - Je ni kweli Wafaransa hawapendi kazi na ni wavivu? 00:45:08 - Ushauri kwa mtu anayependa kuja kusoma na kufanya kazi Ufaransa na Ughaibuni kwa ujumla. 00:49:08 - Je, kodi kubwa ya nchini Ufaransa ni kikwazo kwako? 00:50:39 - Maadili ya Kifaransa ambayo yanaweza kuleta faida pia Tanzania 00:52:52 - Kulinganisha mtazamo wa Kazi na Mafaniko kati ya Tanzania na Ufaransa. 00:55:59 - Mitazamo binafsi iliyomfanya Felician Matinya afanikiwe kwenye safari yake ya kitaaluma na maisha nchini Ufaransa. 00:58:49 - Vitu gani toka Tanzania vimekusaidia kufikia malengo yako Ughaibuni? 01:00:41 - Ushauri kwa serikali na Vyuo Vikuu Tanzania juu ya kuboresha elimu na mitaala ili kutoa vijana wenye uwezo wa kushindana Kimataifa. 01:04:09 - Je, unafikiri kurudi nyumbani Tanzania siku moja? 01:05:55 - Changamoto za kufanya re-integration baada ya kutoka Ughaibuni na kurudi Tanzania kama mtaalamu 01:09:07 - Ushauri kwa Watanzania wanaorudi nyumbani kujenga network ili kushiriki vyema katika kuendeleza gurudumu la maendeleo Tanzania 01:09:40 - Fursa za ujasiriamali nchini Ufaransa, zimekaaje? 01:11:35 - Urahisi katika kufungua kampuni na kufanya ujasiriamali nchini Ufaransa. 01:12:40 - Umuhimu wa lugha kwa mjasiriamali. 01:13:01 - Ujumbe muhimu kwa vijana wanaotaka kuja kufanya maisha yao Ughaibuni, hasa Ufaransa. 01:14:55 - Je, kama safari yako ingekuwa kitabu, ungekipa jina gani? 01:15:55 - Umuhimu wa kupenda kusoma katika kuhimili mabadiliko ya maisha na kuishi ughaibuni. 01:18:36 - Baadhi ya vitu vinavyompendeza Felician nchini Ufaransa. #SogaZaDiaspora #MaishaUghaibuni #KaziUlaya #KaziUfaransa #WatanzaniaUghaibuni #DiasporaLife #UkweliKuhusuUlaya