У нас вы можете посмотреть бесплатно Nini baada ya Ramadhani ماذا بعد رمضان؟ 🔴 LIVE DARSA Ust. Hassan A Hakeem Saeed или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Darsa ilifanyika Shawwal 15, 1446 H Jumapili April 13, 2025 ماذا بعد رمضان؟ Nini baada ya Ramadhani? Tumeuaga mwezi wa Ramadhano, tumeuaga mwezi wa Qur-aani, mwezi wa takwa, mwezi wa jihad, mwezi wa maghufira, mwezi wa dua, mwezi wa kutolewa watu Motoni. Kila Muislamu aliyeingia katika mwezi wa Ramadhani atakuwa ameingia na ametoka katika madrasa ya takwa. Na mtu anapoingia katika madrasa yoyote ile, hutoka humo akiwa ametunukiwa shahada ya lile somo alilolisoma, na baada ya hapo huitumia ile elimu aliyoisoma kumsaidia katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Hivyo basi ni vyema kwa Muislamu ni vyema aendelee na kushikamana na yale aliyoyapata kwenye Ramadhani hadi atakapokutana na Rabi wake. Allah Anasema: وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ "Na muabudu Rabi wako mpaka ikufikie yakini (mauti)" Al Hijr : 99. Kinachotakikana kwa Muislamu ni istiqaamah (kuendelea kuwa thabiti/imara) فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ "Basi thibitikeni imara Kwake, na muombeni maghufira" Fusswilat: 6. : أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ الثّقَفيِّ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ: آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)). Kutokana na Abu Amr, vile vile (anajulikana kama) Abu Amrah Sufyan bin Abdillah (Allah Awe Radhi Nae) amesema: Nilisema: Ewe Rasuli wa Allah! Niambie neno katika Uislamu ambalo sitoweza kumuuliza mmoja yeyote yule ghari yako wewe. Rasuli wa Allah akasema:"Sema; Namemuamini Allah, kisha kuwa na istiqamah (mwenye kunyooka; kwa kuendelea kushikamana na ibaada na kuwa na msimamo madhubuti)"Muslim. Kuhakikisha kuwa umewafikishwa kuweza kufikia kuwa na istiqamah, ni vyema jiulize maswali yafuatayo: 1. Je, unaendelea kufunga (kuna Saumu nyingi tu za Sunnah)? 2. Je, unaendekea na kisimamo cha usiku (Qiyamul-Layl)? 3. Je, unaendelea na usomaji na usikilizaji wa Qur-aani? 4. Je, unaendelea na uombaji wa dua? 5. Je, unaendelea na kububujikwa na machozi kwa kukumbuka dhambi zako na kuihofu adhabu ya Allah? Ni vyema ieleweke kwamba Allah Anapenda amali zinazoendeleza japokuwa ni chache kuliko amali nyingi zisizokuwa zenye kuendelezwe: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((أَحَبَّ الْأَعْمَالِ إِلَى اللَّهِ أَدْوَمُهَا وَإِنْ قَلَّ)) متفق ع Rasuli wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: "Amali zinazopendaza zaidi kwa Allah ni zile zinazodumishwa japokuwa ni kalilii". Wamewafikiana Bukhari na Muslim. (Ee Allaah! Ee Muelekezaji wa nyoyo, Elekeza nyoyo zetu katika utii Wako