У нас вы можете посмотреть бесплатно KILIO CHA BABA MTU, Daktari Mlevi Aliyosababisha Kifo cha Zainabu, Tamko Zito Latolewa Tunduru или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa majina ya zainabu Kazembe boma mkazi wa kata ya Malumba halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma amefariki dunia ikielezwa kuwa ni uzembe wa daktari wa zahanati ya Malumba ambaye alifika kumuhudumia mgonjwa huyo akiwa amelewa pombe. Akimuelezea mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma ndugu Oddo Mwisho bwana Abdala Manjoro baba mkwe wa marehemu Zainabu Kazembe Boma mkazi wa kata ya Malumba iliyopo halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma amesema kuwa tukio la kufariki mkwe wake linaelezwa kuwa ni la uzembe wa daktari wa zahanati ya Malumba ambalo lilitokea tarehee 8/1/2025 inaelezwa kuwa mwanamke huyo alifariki dunia baada ya kuugua ghafla na akakimbizwa katika zahanati ya Malumba na baada ya kufika hapo mganga wa hospitali hiyo anayefahamika kwa majina ya Ignas Magomba muda huo hakuwepo katika zahanati hiyo na alifika baada ya saa moja huku akiwa amelewa na akamuhudumia mgonjwa kwa kumuwekea dripu kisha akaondoka na hali ya mgonjwa ikaendelea kuwa mbaya ilipofika saa nne usiku walipomfuata tena daktari huyo alishindwa kuamka kutokana na uchovu uliosababishwa na pombe alizokunywa na akarudi katika zahanati hiyo saa 11 asubuhi huku mgonjwa akiwa katika hali mbaya na akafariki dunia. Akithibitisha kutokea tukio la mwanamke kufariki linaloelezwa kuwa ni uzembe wa daktari wa zahanati ya Malumba diwani wa kata ya Malumba mhe Said Makunganya amesema ni kweli tukio hilo limetokea na alipoongea na daktari huyo alimjibu kuwa alizidiwa na pombe na alipofika nyumbani akapitiwa na usingizi. Baada ya kupokea maelezo hayo mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma ndugu Oddo Mwisho amesema ameichukua changamoto ya uzembe wa daktari huyo na anaipeleka katika sehemu husika ili hatua zichukuliwe huku viongozi wakitakiwa kusikiliza kero za wananchi mara kwa mara ili waweze kujua changamoto zao wananchi ambao wanawaongoza. #BmtvTanzania #Bmtv Tembelea https://bmtvtanzania.com/ INSTAGRAM / bmtvtanzania FACEBOOK / bmtvtanzania TWITTER / bmtvtanzania1