У нас вы можете посмотреть бесплатно 🔴 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana wa JKT ambao walifukuzwa kwa utovu wa nidhamu tarehe 12/04/2021. Akiongea na Wanahabari Jijini Dar es salaam, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, amesema Vijana hao ambao idadi yao ni 854 ambapo mmoja amefariki Dunia na kufanya idadi ya waliopo kuwa 853 wamepata Msamaha huo baada ya Jeshi Kufanya uchunguzi na utafiti wa kina na kubaini kuwa vijana hao walifanya vitendo hivyo vya ukiukwaji wa nidhamu, na kwamba Mkuu wa Majeshi Jenerali Salvatory Mabeyo amejiridhisha kuwa wengi wao walifanya hivyo kutokana na Utoto wao, Kutokujitambua, Kufuata Mkumbo na wengine Kurubuniwa. Baada ya uchunguzi huo, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limejiridhisha pasipo na shaka juu ya mwenendo wa vijana hao ni wa kuridhisha na limeona wanastahili Msamaha huo na linawaomba Umma wa Watanzania kuendelea kuwaamini Vijana hao na kuwapa nafasi nyingine tena ili waendelee na Mafunzo. Katika maelekezo hayo, Mkuu wa Majeshi ameelekeza Vijana hao waliopewa msamaha wakaripoti Kambi ya 841 Mafinga Mkoani Iringa kabla au ifikapo tarehe 12/03/2022. Hata hivyo onyo limetolewa kwa yeyote ambaye sio sehemu ya vijana hao kutokujaribu kughushi ama kuripoti kwenye kambi hio kwani Majina na Taarifa za vijana wote zipo na zimehifadhiwa, na kwa yeyote atakayethubutu kufanya hivyo atachukuliwa hatua stahiki.