У нас вы можете посмотреть бесплатно MATIBABU UKIUMIA/KUTEGUKA GOTI: Kujitibu mwenyewe nyumbani или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kano (ligaments) za kwenye goti zinaweza kutika, kuteguka au kukatikaka kabisa. Kuumia kwenye goti, namna ya matibabu yake ni tofauti sana ukilinganisha na mtu aliyeumia kifundo cha mguu (ankle). Kama umeumia na kano za kwenye goti zimekatika utahitajika kufanyiwa upasuaji mapema sana ili kuzirekebisha. Kama ukichelewa kufanyiwa matibabu, upasuaji unakuwa mgumu zaidi na matokeo yake huwa sio mazuri kama inavyotarajiwa. Na hii ndiyo sababu tunayaendea kwa umakini sana matibabu ya goti ukilinganisha na matibabu ya mtu aliyeumia kifundo cha mguu. Kama kuna wasiwasi wowote kwamba kano yoyote imekatika, nenda kaonane na daktari mapema. Mifupa ya kwenye kifundo cha mguu ni rahisi kuvunjika, lakini ni nadra sana kukuta mifupa ya kwenye goti imevunjika; kama mfupa wa kwenye goti umevunjika, utahitajika kutibiwa na daktari pia. Watu wengi wanaumia kwenye goti wanapokuwa wanashiriki michezo, huu ndio wakati ambao mtu anaweza kukunja goti vibaya au kupigwa, kugongana au kugongwa kwenye goti. Unaweza kupata jeraha kubwa na hatari sana kama mguu utakuwa umekanyaga chini kwa nguvu, halafu mtu akakukanyaga kwenye goti kutoka upande. Kama mguu hautasogea, kuna hatari kubwa kwamba, goti lako litaumia vibaya sana. Kama wewe ni mwanamichezo, ni kweli kwamba, hakuna njia ya uhakika ya kuepuka hali hii. Wapo wanamichezo wanaojaribu kuvaa knee braces na supports, lakini hazina msaada sana. Mjongeo usio wa kawiada Kano za kwenye goti zinapokuwa zimekatika, mguu utakuwa unacheza kutoka upande mmoja mpaka mwingine mguu unapokuwa wima. Jaribu kulinganisha goti lililoumia na goti la upande mwingine uone mguu unacheza kiasi gani. Kama goti limeteleza kwenda nyuma (the drawer sign) hii inaashiria kuwa kano iliyo mbele ya goti imekatika na hii si hali ya kawaida. Kama unadhani goti linachezacheza, nenda kamwone daktari. Kama gegedu la kwenye goti limechanika, inaweza kuzuia goti lako kujongea, unaweza ukashindwa kukunjua goti. Sio lazima kufanyiwa upasuaji mara tu baada ya gegedu kuumia, lakini unahitaji kumwona daktari. Maumivu na kuvimba Kupata maumivu na kuvimba sana kwenye goti hakuashirii kwamba jeraha lako ni baya sana, kwa hiyo usihofu sana. Jambo la muhimu zaidi a kuangali ni kama unaweza kukanyaga na goti lililoumia na kuangalia kama goti linajongea vizuri bila kukwama na kwamba goti halichezichezi unapolitikisa (hii ni muhimu zaidi kuonesha ukubwa wa tatizo) Kwa hali ya kawaida kuvutika na kuteguka kwa goti kunasababisha maumivu hapo hapo na maumivu haya yanendelea kuwepo kwa masaa na hata siku kadhaa baada ya kuumia. Kuvimba huwa kunaanza taratibu kwa masaa kadhaa na uvimbe unaweza kukuogofya sana. Kama kuna kano imekatika, utahisi maumivu makali sana muda huo huo, na baada ya muda maumivu yatapungua sana au na hata kuisha kabisa baada ya muda. Mara nyingi utakuta kuna damu inavujia ndani kuzunguka mahali ilipokatika hiyo kano (ligament), sehemu hiyo inavimba haraka sana na kuwa kubwa mpaka kukushangaza. Mpango bora unapokuwa na jeraha kwenye goti, epuka kufanyisha kazi goti lako mpaka pale utakapokuwa na uhakika kuwa jeraha ulilonalo si kubwa. Matibabu ninayokwenda kuyazungumza hapa (matibabu ya nyumbani) ni kwa ajili ya watu wenye majeraha madogo yaliyosababisha kuvutika au kuteguka kwa kano za goti pekee. Kama kano imekatika onana na daktari. Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani ukiumia goti Kwanza pumzisha goti na liinue. Chukua barafu, uifunike kwa kitambaa na kisha iweke kwenye goti kwa dakika 30 ili kupunguza uvimbe. LKKama unaona uvimbe unaendela kuongezeka japo umepumzisha mguu na kuweka barafu, ni vizuri kumwona daktari. Kama hali ni shwari, endelea kuweka barafu dakika 30 kisha upumzishe mguu kwa dakika 15 na kisha uweke tena barafu kwa dakika nyingine 30 kwa masaa kadhaa ya mwanzo. Unaweza kujaribu kusimama mara kadhaa huku ukiangalia hali ya maumivu na kuvimba ikoje. Baada ya masaa 24 tunategemea goti lako litakuwa limeanza kuwa vizuri na kurudi kwenye hali yake. Baada ya masaa 72 inatakuwa uwe umekuwa vizuri kabisa, kama sivyo nenda kamwone daktari. Lakini pia ni vizuri kukumbuka kwamba, kuvutika au kuteguka kwa kano za goti zinahitaji zaidi ya wiki 4 mpa 6 kupona kanibisa, kwa hiyo unapaswa kulinda goti lisiumie zaidi. Tumia elastic bandage kufunga goti ili kulilinda. Unaweza pia kutumia dawa za kupunguza maumivu kama acetaminophen, ibuprofen au naproxen ili kupunguza karaha. Kwa daktari Kama ukiamua kwenda kwa daktari, daktari atakufanyia uchunguzi wa goti, atapiga picha ya eksirei (japokuwa mara nyingi hazina msaada wowote), kama kano imekatika atakufanyia upasuaji kuirekebisha, na kama kuna damu nyingi imevuja kwenye goti, anaweza kutumia sindano kuivuta na kuiondoa. Kwa wale ambao majeraha yao yataonekana ni madogo, watashauriwa kutumia matibabu ya nyumbani niliyoyaeleza awali. https://wikielimu.org