У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 11/03/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 11/03/2026 MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 19 NENO KUU: Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; MADA: "KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON) UJUMBE WA LEO: NAMNA NYAKATI NGUMU KWENYE MISIMU ZINAVYOWEZA KUTENGENEZA WATU WA KUSUDI. B. Wekeza kwenye maombi ya kuombea kibali chako na kusafisha nyota yako. Kuna wakati kinachosababisha ukataliwe ni vita ya ulimwengu wa roho, hivyo tumia muda wako wa kukataliwa na kutengwa kukaa faraghani kwenye maombi kuutengeneza mvuto wako, kibali chako na nyota yako. Esta 5 : 1 - 3 Esta alikataliwa na hakukutana na mume wake kwa siku 30, lakini baada ya maombi kibali chake kilirejeshwa na akaahidiwa zawadi ya thamani kubwa (hata nusu ya ufalme nitakupa). Kukataliwa ni vazi analoweza kuvalishwa mtu ili asikubalike popote anapoenda, hivyo unapoomba elewa kwamba Yesu alikataliwa kwaajili yako na anaweza kukuvua hilo vazi la kukataliwa. Isaya 53 : 3 - 5 Badala ya kuhuzunika na kusikitika kwasababu ya kukataliwa na kudharauliwa, mtangazie shetani kwamba Yesu alishayachukua masikitiko yako na huzuni yako na kwamba utatokea ukiwa na kibali na mvuto machoni pa wote wanaokuona. Wakati mwingine kukataliwa ni roho inayolenga kuua kusudi kubwa la Mungu ndani ya mtu, hivyo omba kwa juhudi wala usijikatie tamaa. MAMBO YANAYOFANYIKA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO KUMFANYA MTU AKATALIWE. a. Kuiharibu kazi anayofanya mtu. Kazi ya mikono ya mtu inaweza kuharibiwa ili mtu apoteze kibali kwa watu. Mathayo 7 : 15 - 16 Kujihadhari maana yake ni kujitenga nao / kuwakataa. Unaweza kukataliwa kwasababu ya ulichozalisha. b. Kumshambulia mtu kwa magonjwa. Magonjwa hasa mahali pa kazi yanakufanya upoteze kibali. 1Samw 30 : 13 Ugonjwa ni silaha inayotumika kwenye ulimwengu wa roho kumfanya mtu akataliwe na kutengwa, hivyo unapoombea kibali chako kwenye eneo fulani, ombea pia afya yako. c. Kuishambulia tabia ya mtu. Adui anaweza kumfunika mtu na tabia mbaya kama za ulevi, uzinzi, au kumuwekea maneno mabaya kinywani, majibu mabaya ili kukiharibu kibali chake mbele za watu. Esta 1 : 12, 15 - 19. Kila tabia mbaya inapelekea mtu kutengwa. Mithali 22 : 24 d. Kumfunika mtu kwa kitambaa au leso ya kichawi kwenye paji la uso. Unaweza usikubalike kwa chochote kwasababu uso wako umefunikwa kichawi. Yohana 11 : 44. Mhubiri: Mwl. Andrew Bartimayo Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com