У нас вы можете посмотреть бесплатно MTAKA APINDUA MAAMUZI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE ''WAGONJWA SIO FURSA'' или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WAGONJWA SIO FURSA YA BIASHARA 'RC MTAKA' MAKETE. Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametengua uamuzi wa halmashauri ya Wilaya ya Makete kuzia mabasi kushusha na kupakia abiria katika hospitali ya Consolata Ikonda akieleza uamuzi huo kua haukuzingatia utu na kuwajali wagonjwa wanaofika hospitalini hapo Kupatiwa Matibabu. Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya hospitali hiyo Mkurugenzi Father William Mkalula Na Lazaro Mchami Daktari wa Hospitali hiyo pamoja na wagonjwa wamesema maamzi ya awali yalikuwa yanawaumza wagonjwa wanaofika katika hosptali hiyo kutibiwa kulingana na hali ya uchumi ambapo walikuwa wakichajiwa shilling elfu Moja hadi elfu tatu ili waweze kufikishwa hospitalini hapo. Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akamhoji mkurugenzi wa wilaya ya Makete Bw.William Makufwe ikiwa kuna kubaya madhara wagonjwa kushishwa katika hospitali hiyo. Kabla ya maamuzi rasmi kutolewa kikaitishwa kikao cha faragha cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na mkoa ili kujadili na kutoka na maamuzi ya kuridhia abiria kupanda na kushushwa katika hospitali hiyo na hapa Mkuu wa Mkoa anatoa majibu ya Kikao hicho kilichochukua Zaidi ya dakika 30 ili kufikia maamuzi ambapo kuanzia Leo 6 March 2024 mabasi kuanza kushusha na kupakia na kushusha katika hosptali hiyo. Rehema Chaula na huruma Emanuel ambao ni wananchi waliofika kupata huduma ya matibabu katika hospitali ya Consolata Ikonda wamesema hatua hiyo itawasaidia wananchi ambao wamekuwa wakitapeliwa na waendesha bodaboda na bajaji kwa kutozwa bei ya shilingi elfu moja mpaka elfu tatu kutoka Sitendi ya Tandala-Hosptali ya Ikonda. Mwenyekiti wa madereva wa vyombo vya usafirishaji wilaya ya Makete Bw Joseph Mansela amesema maamuzi ya kuruhusu abiria kupanda na kushushwa hospitali hapo kimekuwa kilio chao cha muda mrefu na kwamba wanaimani wataweka utaratibu mzuri usiowapeleka usumbufu wa wagonjwa. Maamuzi hayo yanatolewa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe ya kutembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe.