У нас вы можете посмотреть бесплатно SHAIRI LA WATOTO | KILELE CHA MAADHIMISHO YA WATOTO TAG 2025| TAG KIMARA CHURCH или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya watoto TAG 2025. Shairi hili limeandaliwa na watoto TAG Kimara church, likisimamiwa na mwalimu wao Lucy Sungusia. SHAIRI 1. Tunamshukuru Mungu, kufikia mwaka huu, Sisi watoto wa Mungu, kwa Baraka zake kuu, Tunaishi kwa undugu, timiza agizo kuu, Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 2. Tumemsoma Yusufu, mtoto mwaminifu, Alikuwa mtiifu, babaye alimsifu, Ndugu walikashifu, Mungu kampa Utukufu Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 3. Naye mtoto Samueli, kawa nabii wa Bwana, Chini ya kuhani Eli,kamtumikia Bwana, Mwamuzi Israeli, Ongoza katika Bwana Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 4. Na mtoto Jeremia, wekwa juu ya mataifa , Kuharibu na kung’oa, kazi zote za Lusifa, Kujenga kumpandia, Bwana kazi zenye sifa, Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 5. Mtoto Yesu liweza, ishi uweza wa Mungu Hekaluni aliweza, jifunza Neno la Mungu, Wanadamu kapendeza, kapendeza na kwa Mungu Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 6. Mafundisho tunapata, watoto na wanafunzi, Yesu tunamfuata, Yeye kwetu mkufunzi, Kanisa tumelipata, Neno ni kama kurinzi Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 7. Wazazi tunawaomba, msiache kutujenga, Njia ya mbingu nyembamba, ni mengi yanatuzonga, Kusoma Neno kuomba, kwa pamoja tutasonga, Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. 8. Walimu twashukuruni, kwa mengi mnatufunza, Wazazi twawashukuru, ni vyema mnatutunza, Na kanisa twashukuruni, ni mengi tunajifunza, Sasa ni wakati wetu, kumtumikia Mungu. "Ungana nasi kumwabudu Mungu live kila Jumapili. Ibada ya kwanza huanza 12:00 asubuhi na ibada ya pili 04:00 asubuhi. Kanisa letu lipo Kimara Mwisho, mwendo wa dakika moja kutoka Morogoro Road. Pia tufuatilie katika mitadao ya kijamii; Instagram @tagkimara / tagkimara Facebook @TAG-Kimara Church / kimaratag Ubarikiwe!