У нас вы можете посмотреть бесплатно CCM MOROGORO YAPITISHA MAJINA YA WAGOMBEA UDIWANI, 11 WAKWAMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Morogoro. Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimeketi jana Agosti 13, 2025 kujadili na kupitisha majina ya wanachama watakaogombea nafasi za udiwani wa kata na viti maalumu. Katika kata 214 wanachama 203 wameteuliwa kuwania nafasi hizo, huku kata 11 zikipelekwa kwenye hatua ya uhakiki utakaofanywa na Sekretarieti ya Halmashauri kuu CCM Taifa ili kuhakikisha haki inatendeka. Akizungumza leo Agosti 14, 2025 Katibu wa CCM mkoani humo, Nuru Ngereja amesema miongoni mwao wagombea 11 wapo waliokuwa vinara kwenye kura za maoni ambao wanatuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo za kimaadili na makundi, hivyo tathmini ya kina itafanywa ili kubaini ukweli. Kata zilizoko kwenye uhakiki ni Mwembesongo, Mafiga, Mbuyuni, Kilakala, Lukobe, Mlimani na Mindu zote za Manispaa ya Morogoro, Mtimbira (Malinyi), Ngerengere (Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro), Msolwa Stesheni (Kilombero) na Mlali (Mvomero). (Imeandikwa na Jackson John).