У нас вы можете посмотреть бесплатно HASUNGA ASISITIZA BUSARA BADALA YA MABAVU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Jimbo la Vwawa, Japhet Hasunga, alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kikao muhimu kilichowakutanisha wafanyabiashara wa Soko la Ichenjezya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega. Kikao hicho kililenga kujadili na kutafuta suluhisho la changamoto zilizoibuka kufuatia hatua ya kufungwa kwa maduka ya wafanyabiashara katika soko hilo. Akitoa maoni yake katika kikao hicho, Mheshimiwa Hasunga alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya wazi, ya heshima na yenye kujenga, kama msingi wa utatuzi wa migogoro kati ya wafanyabiashara na mamlaka husika. Alieleza kuwa wafanyabiashara ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa eneo hilo na Taifa kwa ujumla, hivyo ni vyema kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa rafiki, salama na yanayozingatia sheria bila kuathiri ustawi wa wananchi. Huku akiweka msisitizo wakwamba suala la ulipaji kodi ni jukumu la kila mfanyabiashara na mtanzania ili kukuza taifa na kuleta maendeleo . Aidha, Mbunge huyo alibainisha kuwa hatua ya kufunga maduka, si sawa kisheria na kisera inapaswa kuambatana na mashauriano ya kina ili kuepusha madhara makubwa ya kiuchumi kwa wafanyabiashara na familia zao. Kwa ujumla, kikao hicho kilionesha dhamira ya pamoja ya kutatua changamoto kwa njia ya maelewano, huku kikiweka msisitizo katika kujenga mazingira bora ya biashara yatakayochochea ukuaji wa uchumi wa eneo la Ichenjezya na Wilaya ya Mbozi kwa ujumla. Na Mwishowe maduka yote yalifunguliwa . #skytv