У нас вы можете посмотреть бесплатно VIJANA MOSHI WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA FEDHA ZA UWEZESHAJI WA WATENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Vijana wanaotengeneza maudhui ya mtandaoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba fedha za uwezeshaji zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kusaidia watengeneza maudhui ya mtandaoni, kukuza vipaji na kujiajiri. Fomu hizo zinatolewa katika Ofisi za Kitengo cha Mawasiliano Serikalini zilizopo Halmashauri, ambapo tangu kutangazwa kwa fursa hiyo, kumeshuhudiwa mwamko wa vijana wanaojishughulisha na utengenezaji wa maudhui ya kidijitali ikiwemo video, picha, makala, podikasti na maudhui ya mitandao ya kijamii. Akizungumza wakati wa kuwakabidhi fomu hizo Afisa Habari na Mawasiliano Emanuel Kessy amesema lengo la mpango huo ni kuwawezesha vijana kutumia teknolojia na ubunifu kama njia ya kujiajiri, kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza mchango wao katika uchumi wa kidijitali. “Serikali inatambua mchango mkubwa wa vijana kwenye sekta ya maudhui mtandaoni. Kupitia fedha hizi, tunatarajia kuona ubunifu unaokua, ajira mpya zikizalishwa na vipaji vya vijana wa Moshi vikifika mbali zaidi,” amesema Kessy. Baadhi ya vijana waliochukua fomu hizo wamesema hatua hiyo ya Serikali ni kichocheo kikubwa kwao kuboresha kazi zao, kununua vifaa vya kisasa pamoja na kupanua wigo wa maudhui wanayozalisha ili yaweze kushindana kimataifa. Mpango huu ni sehemu ya jitihada za Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua vijana kiuchumi, kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani na kujenga taifa lenye vijana wabunifu, wanaojitegemea na wenye mchango chanya kwa jamii.