У нас вы можете посмотреть бесплатно Wavuvi wabaki ‘dilema’ Ziwa Tanganyika likifungwa leo или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Baadhi ya wavuvi wa mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi inayozungukwa na Ziwa Tanganyika wamesema hawajui hatma yao baada ya ziwa hilo kufungwa leo Mei 15 na kufunguliwa Agosti 15, 2024 ili kutoa nafasi kwa samaki kuzaliana. Serikali kupitia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ilisema kufungwa kwa ziwa hilo ni Makubaliano ya kusimamisha shughuli za uvuvi kwa kipindi hicho yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Nchi hizo zilikubaliana kutambua zana haramu za uvuvi ili kuruhusu mazalia ya samaki kwa wingi na kudhibiti uvuvi haramu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa kulipumzisha ziwa kutokana na shughuli za uvuvi kila mwaka kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15 kwa miaka mitatu mfululizo. Hatahivyo mwaka 2023 Serikali ilisitisha uamuzi wa kufunga ziwa hilo baada ya malalamiko ya wadau wa uvuvi kulalamikia kutoshirikishwa, lakini mapema mwaka huu ilitangaza tena uamuzi huo. Wakizungumza na Mwananchi Digital wavuvi wa ziwa hilo wamesema baada ya kufungwa ziwa hilo hali yao ya maisha itakuwa mbaya zaidi kwakuwa tayari wameshapata majanga ya mafuriko. Kiongozi wa Wavuvi Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Malius Kiluba amesema kikubwa kinachokithiri ziwani humo na kutakiwa kifanyiwe kazi ni uvuvi haramu akidai hata wizara hiyo inajua lakini haijazuia badala yake imekimbilia kufunga ziwa. Mkuzaji wa viumbe maji mkoani Kigoma, Alexander Elikado amesema Samaki wataongezeka ila kwa jamii inayotegemea ziwa uchumi lazima ushuke. Akichangia taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato ya matumizi ya fedha ya mwaka 2024/25 ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani ameshauri kabla ziwa hilo halijafungwa itafutwe njia ya kupambana na uvuvi haramu akidai ndio chanzo cha samaki kupungua. Ameongeza kuwa hata ugawaji vizimba unaoendelea kama mbadala wa ziwa kufungwa maandalizi yalipaswa kufanywa tangu mwaka jana akitaka elimu ya maandiko ya kuomba vizimba itolewe pamoja na kutengeneza mazingira mazuri kwa wavuvi. Ziwa Tanganyika lina ukubwa wa kilometa za mraba 32,900 huku Tanzania ikimiliki kilometa za mraba 13, 489, sawa na asilimia 41 ya ziwa lote.