У нас вы можете посмотреть бесплатно EACOP KUSHIRIKIANA NA GASCO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kufuatia kukaribia kukamilika kwa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), yaani East African Crude Oil Pipeline, uongozi wa EACOP umeamua kufanya maandalizi ya uendeshaji wa mradi kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), GASCO. Kupitia ushirikiano huo, GASCO itatoa mafunzo ya uzoefu wa vitendo katika uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya Gesi Asilia. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wataalamu wa EACOP uwezo wa kitaalamu na kiutendaji katika kusimamia miundombinu mikubwa ya nishati kwa ufanisi, usalama na kuzingatia viwango vya kimataifa. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ujuzi wa ndani, kuimarisha ubadilishanaji wa maarifa kati ya taasisi hizo, na kuweka msingi imara wa uendeshaji endelevu wa miundombinu ya mradi wa EACOP mara tu utakapokamilika rasmi.