У нас вы можете посмотреть бесплатно Rais Samia Suluhu Hassan amemkosoa mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais Samia Suluhu Hassan amemkosoa mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, mbele ya wapigakura wake kwa kile alichokieleza kuwa ni tabia ya kutafuta umaarufu badala ya kutekeleza majukumu ya msingi ya uwakilishi wa wananchi. Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Juni 17, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Meatu, mkoani Simiyu, baada ya Mbunge Mpina kueleza matatizo ya jimbo lake akimtaka Rais kuyashughulikia. Akijibu hoja hizo, Rais Samia amesema, "Ndugu zangu, maombi kama haya yamekwishawasilishwa bungeni na mawaziri wakatekeleze. Kuleta maombi haya hapa kwenye mkutano wa Rais ni kujitafutia umaarufu na kuthibitisha kuwa Mbunge hakulifanyia haki jimbo lake." Rais Samia Amefafanua kuwa matatizo ya maendeleo katika jimbo kama ujenzi wa madaraja ni mambo ya kawaida yanayopaswa kushughulikiwa na wizara husika kupitia hoja na ushawishi wa mbunge bungeni, si kwa mikutano ya Rais. Amemshangaa Mbunge huyo kwa kutumia muda mwingi kuzungumzia miradi ya kitaifa kama Bwawa la Julius Nyerere na Reli ya Kisasa (SGR), badala ya kueleza kwa kina changamoto za Kisesa. Kwa mujibu wake, hali hiyo inaonesha kuwa Mpina ana mawazo ya kitaifa zaidi, na huenda angefaa kuwa Mbunge wa kuteuliwa kupitia nafasi 10 za Rais, badala ya kuwakilisha jimbo moja.