У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI WA ULINZI AONGOZA UPANDAJI MITI MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA NA VIWANJA VYA WATUMISHI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 31 Januari 2025, amewaongoza Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo eneo la viwanja vya makazi ya watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Chinangali 2 nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti, Mhe. Waziri wa Ulinzi na JKT, amesema zoezi hilo ni muendelezo wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ya upandaji miti mwezi Januari ya kila mwaka. Kabla ya kuhitimisha hotuba yake, Waziri Dkt. Stergomena Tax, ameipongeza Kamati ya Mradi wa Viwanja vya Watumishi kwa kuratibu na kusimamia zoezi hilo tangu mwanzo mpaka hatua ya kukabidhiwa hati ya umiliki wa viwanja kwa watumishi na ameahidi kuwaunga mkono kwa kuwanunulia matanki ya maji ili kutatua changamoto ya uhifadhi wa maji ya kisima kilichopo. Zoezi la Upandaji miti ya matunda na kivuli katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, lilihudhuriwa pia na Mkuu wa Tawi la Manunuzi na Uhandisi, Meja Jenerali Hawa Kodi na baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi pamoja na Makamishna toka Makao Makuu ya Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wa Umma ambao pia walishiriki upandaji miti. Akielezea maendeleo ya Mradi wa Viwanja vya Watumishi wa Wizara, Mratibu na Mwenyekiti wa zoezi la Mradi wa viwanja vya Watumishi, Kamishna wa Sera na Mipango Bw. Obedi Sayore, amefafanua kuwa muitikio umekuwa mkubwa wa uhitajio wa viwanja kwa watumishi na kueleza ukubwa wa eneo la Mradi ni ekari 244 na idadi ya viwanja ni 504 Akizungumza kwa niaba ya Wanufaika wa Mradi, Bw. Abdul Yasin ameishukuru Kamati kwa uratibu wa upatikanaji viwanja hivyo maeneo ya Chinangali 2 kwa ajili ya makazi ambayo yatakuwa karibu na mazingira ya kazini katika eneo la Kikombo. #wizarayaulinzi #jwtz #jkt