У нас вы можете посмотреть бесплатно PAPA FRANCIS ALIKATAA KABURI LAKE LISIREMBWE, KUZIKWA NDANI YA KANISA HILI… или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Vatican. Taarifa iliyotolewa na Vatican inaeleza kuwa kabla ya kufariki Papa Francis (88) aliugua ugonjwa wa Kiharusi (Stroke) hali iliyosababisha moyo kushindwa kufa kazi huku ikidokeza kuwa madaktari walifanya jitihada kurudisha moyo kufanya kazi lakini ilishindikana. "Papa amefariki kutokana na Stroke,” inaeleza sehemu ya taarifa rasmi ya sababu ya kifo cha Papa Francis iliyochapishwa katika ukurasa rasmi wa Vatican. Pia hati ya kifo cha kiongozi huyo wa kiroho imetaja magonjwa mengine yaliyokuwa yanamsumbua, Papa Francis kuwa ni pamoja na homa ya mapafu (Nimonia), kushindwa kupumua, shinikizo la juu la damu na ugonjwa wa Kisukari. Kwa taratibu za kimatibabu ugonjwa ambao mgonjwa huwa anakuwa nao muda mfupi ama Saa chache kabla ya kifo chake ndio huwa unatajwa kwenye cheti cha kifo kama sababu ya kifo. Baada ya hapo ndio kifo cha Papa hutangazwa. Papa Francis alifariki jana Jumatatu, asubuhi akiwa na umri wa miaka 88. Katika hatua nyingine, wakati wakristo wakiendelea kuomboleza, wosia wa mwisho wa Papa Francis umeeleza jinsi utaratibu wa mazishi yake utavyokuwa. Katika wosia huo, Papa Francis ameeleza kwamba, lazima azikwe katika Kanisa Kuu la Bikira Maria lililoko Roma, Italia haliko Vatican ambako mapapa wengi wamekuwa wakizikwa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. "Miserando atque Eligendo Kwa jina la Utatu Mtakatifu. Amina. Katika maisha yangu nimekuwa nikimtumainia Mama Bikira Maria daima, kwa sababu hii nizikwe kwenye kanisa hilo nikisuburi kufufuliwa siku ya Ufufuo", imesema tarifa hiyo. Papa Francis amekuwa akiishi maisha ya ufukara hali ambayo ameisisitiza kuhusu maziko yake kuwa yazingatie alichoandika katika wosia wake. Wosia wake unaeleza kwamba, mazishi yake yasiwe ya kifahari na wala kaburi lake lisiwe na mapambo yoyote isipokuwa liandikwe jina lake tu la ‘Fransicus’. Kuhusu gharama za maziko, wosia wa Papa Francis umeeleza kuwa, gharama zote zimetolewa na mfadhili ambaye hakutajwa jina na zimekabidhiwa kwa Kardinali, Rolandas Makrickas. Mwisho wa Wosia wake Papa amesema, "Mola awape thawabu ifaayo wale wote walionipenda na wanaoendelea kuniombea. Mateso ambayo yamenizonga katika kipindi cha mwisho cha maisha yangu, nayatoa kwa watu, kwa ajli ya amani duniani na udugu kati ya undugu kati ya mataifa.” Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa mashirika ya habari.