У нас вы можете посмотреть бесплатно NHIF YALENGA KUGUSA KAYA ZISIZO NA UWEZO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imekuja na mpango wa 'Bima ya Afya kwa wote' ambapo kupitia mpango huo Serikali itazisajili kaya zisizo na uwezo na kuziwezesha kupata kadi za matibabu ambazo zitawawezesha kupata matibabu zaidi ya 300 kwa kutumia kadi za NHIF. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Bima ya Afya kwa wote Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Khamana Simba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Wananchi na kuwarahishia kupata huduma Bora za matibabu. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mhe. Shafy Kanefuka amesema kuwa Bima ya Afya kwa wote ni miongoni mwa ahadi ambazo zilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Kampeni na ameitekeleza kwa vitendo hivyo ni fursa kwa Wananchi kujiandikisha na kupata matibabu kwa gharama nafuu. Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Ndg. Saida Mahugu amewaasa Wananchi kujiandikisha ili kupata bima ya Afya kwani kwa kufanya hivyo Watajihakikishia kupata matibabu wakati wote hata kwa nyakati ambazo fedha zimekosekana. Mbali na kaya zisizo na uwezo, ikumbukwe Bima hiyo inahusisha Jumla ya wanakaya sita ambao watapata matibabu kwa kipindi cha Mwaka mzima kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini.