У нас вы можете посмотреть бесплатно KILICHOTOKEA TAZARA BAADA YA ABIRIA WA TRENI KUSHINDWA KUSAFIRI TANGU JANA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Abiria wanaotumia usafiri wa treni kupitia reli ya Tazara kutoka Dar es Salaam hadi Mbeya wameiomba Serikali kuingilia kati usimamizi wa shirika hilo ili kuondoa adha zinazowakumba. Abiria hao wamesema changamoto haziishi kutokana na kukwama mara kwa mara kwa safari, wakieleza wanahisi hali hiyo inatokana na usimamizi mbovu. Wamesema wamekuwa wakipata usumbufu ikiwamo kulala njiani kiasi cha kushindwa kuwahi wanakokwenda. Wameeleza hayo baada ya abiria takribani 250 waliotakiwa kusafiri kwenda Mbeya kutokea Dar es Salaam kukwama kwa saa 24 katika stesheni ya Tazara mkoani Dar es Salaam. Ofisa Uhusiano kwa Umma kutoka Tazara Tanzania, Regina Tarimo amesema kumekuwa na changamoto za mara kwa mara kutokana na uchakavu wa mabehewa. "Si kwamba tunapenda kutesa abiria tuna changamoto ya uchakavu wa mabehewa na pia ni machache kiasi kwamba yanatakiwa kufanyiwa matengenezo mara kwa mara na wakati mwingine yanachukua muda mrefu," amesema. Regina amesema kilichotokea hadi abiria kukwama kuondoka jana Septemba 3, 2024 ni treni kuchelewa kufika Dar es Salaam.