У нас вы можете посмотреть бесплатно MWANZO MWISHO MSUKUMA AFUNGUKA KISA KIZIMA HADI KUGOMBANA NA MUWEKEZAJI GEITA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamati ya Fedha na Uchumi ya Halmashauri ya wilaya ya Geita Imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Kusimamisha shughuli za Ujenzi zilizokuwa zikiendelea kufanywa na Mwekezaji Baada ya kutuhumiwa Kubomoa Baadhi ya Majengo ya Serikali ikiwemo Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Katoro bila kibari Cha Halmashauri kinyume Cha Sheria. Agizo hilo limetolewa mara Baada ya Kamati hiyo Kutembelea na Kukagua eneo hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na Baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakihoji Uhalali wa Mwekezaji huyo Kubomoa Majengo hayo kwa lengo la kutaka kuwekeza bila Makubaliano Kati yake yeye na Serikali ya Kitongoji hicho. Mbunge wa Jimbo la Katoro Mhandishi Kija Ntemi ambaye ni Mjumbe katika Kamati hiyo na Joseph Kasheku Msukumu Mbunge wa Jimbo la Geita ambaye pia ni Mjumbe katika Kamati hiyo wamemtuhumu Mwekezaji huyo Kubomoa Majengo ya Serikali kinyume Cha Sheria huku wakimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kumchukulia hatua kali za Kisheria Kwa upande wake Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Bi. Hongera Edward na Damian Aloys Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro wamekeri kwamba hawajawahi kupata Barua ya kuruhusu Mwekezaji huyo kuvunja Majengo ya Serikali huku na wao wakishangaa kuona Majengo hayo yakiwa yamebomolewa. Rashidi Kwanzibwa ambaye ndiye Mwekezaji na Mtuhumiwa wa Kuvunja Majengo hayo ya Serikali aligoma kuonyesha kibari kilichopelekea yeye kuvunja Majengo ya Serikali huku akiitaka Kamati hiyo kuwasilina na Uongozi wa Chama.