У нас вы можете посмотреть бесплатно KENYA FERRY LAWAMANI? или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KENYA FERRY LAWAMANI? Shirika la Kenya Ferry Services linakosolewa tena baada ya video kusambaa mitandaoni ikionyesha msongamano mkubwa wa abiria katika feri ya MV Likoni kwenye kivuko cha Likoni Ferry. Katika video hiyo ya dakika moja na sekunde ishirini na moja, abiria wanaonekana wakisukumana wakati wa kuingia ndani ya feri. Wengine pia wanaonekana kukaa nyuma ya lango kuu la feri, eneo ambalo kwa kawaida hufungwa wakati safari inaanza ili kuzuia hatari. Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa, kulingana na taratibu rasmi za uendeshaji wa feri, kuna mpangilio maalum wa kupakia abiria na magari pamoja na kufungwa kwa milango ya usalama ili kuzuia ajali kama vile watu au magari kutumbukia baharini. Hata hivyo, hali iliyoonekana kwenye video hiyo inaashiria uwezekano wa ukiukaji wa taratibu hizo. Tukio hili limekumbusha tena mkasa uliotokea mwezi Septemba mwaka 2019, ambapo mama na mwanawe walifariki baada ya gari lao kutumbukia baharini katika kivuko hicho cha Likoni. Baada ya tukio hilo, serikali ilifungua Liwatoni Floating Bridge mwaka 2020 chini ya rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta, kwa lengo la kupunguza matumizi ya feri hata hivyo, daraja hilo halitumiki kwa sasa kulingana na taarifa kutoka duru mbalimbali. Hali hii inaendelea kuibua wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Likoni wanaotegemea feri kila siku, huku wengi wakitaka hatua zaidi zichukuliwe ili kuboresha usalama katika kivuko hicho. #news #mombasa #breakingnews 📡 Watch LIVE on: Al-Haajar Tv 🔴 Website: www.alhaajar.tv 📲 Facebook | YouTube | My Al-Haajar App 🔗 Download the Al-Haajar App today for a seamless viewing experience. Available on both Google Play Store & Apple App Store. 📢 Stay Connected: 📷 Instagram: @alhaajartvkenya 🐦 Twitter (X): @alhaajartvkenya 📘 Facebook: @alhaajartvkenya ▶️ YouTube: @alhaajartvkenya 🎵 TikTok: @alhaajartvkenya 🌎Website: www.alhaajar.tv 🔥 LIKE, SHARE & SUBSCRIBE for more inspiring content! 🔥 ©️ Al-Haajar TV Kenya 2026