У нас вы можете посмотреть бесплатно MACHIFU WAMKARIBISHA MOROGORO SAMIA KWA TAMBIKO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Morogoro: MachiFU wa makabila mbalimbali yaliyopo Mkoani Morogoro, ikiwemo wenyeji Waluguru leo Agosti 28, 2025 majira ya jioni wamekutana kwa pamoja kufanya tambiko maalumu lililolenga kumtakia heri katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan. Tambiko hilo lililo ongozwa na Chief Kingalu Mwanabanzi wa 15, ambaye ndiye kiongozi wa kabila la Waluguru, limefanyika katika mti wa Mtamba uliopo uwanja wa Gofu Manispaa ya Morogoro, ambao kila mwaka hutumiwa na viongozi wa kimila kufanya ibada zao mbalimbali. Siku ya kesho Agosti 29, 2025 Samia anatarajiwa kuanza mikutano ya kempeni Mkoani humo, ambapo ataanzia eneo la Ngerengere Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kisha majira ya mchana ataendelea katika uwanja wa Tumbaku uliopo Manispaa ya Morogoro, siku ya Agosti 30 atafanya mkutano eneo la Sokoine Dakawa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kisha ataelekea Wilaya ya Kilosa ambako atafanya mkutano eneo la shule ya Msingi Kilosa Town na kumalizia ziara yake Mkoani humo kwa kufanya mkutano Wilaya ya Gairo eneo la Villa. Imeandaliwa na Jackson John.