У нас вы можете посмотреть бесплатно KISA CHA BIBI MWENYE KUJIBU MASWALI KWA QUR AN или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ewe Muislamu ulipoumbwa na ukaletwa hapa Duniani uliwekewa katiba na mfumo wa kuishi na njia ya kupita mwanzo mpaka mwisho, nzuri na mbaya, yote hayo utayapata kwenye Qur’an ukifundishwa na Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). KUISOMA QUR'ANI NA ADABU ZAKE Qur'ani Tukufu ni kitabu ambacho ndio msingi wa kufaulu kwenu, chenye kuwatoa watu kwenye giza,na kuwapeleka kwenye nuru, ndani yake kuna khabari ya waliokuja kabla yenu na watakaokuja baada yenu na hakimu kati yenu, chenye kupambanua baina ya haki na batili. Mwenye kukiacha ameumia, mwenye kutaka uongofu kwa hicho ataongoka, na mwenye kutaka kuongoza na kitabu kingine amepotea; ni kamba ya Allah ya kuaminika isiyokatika; ni utajo wa Mwenyezi Mungu ni njia iloyonyoka, mwenye kuifuata hapotei na mwenye kuifuata hachanganyikiwi. Hawashibi nayo wanavyuoni na maajabu yake hayapungui. Atakaye ukweli ataupata humo na mwenye kuhukumu nacho atahukumu kwa usawa. #KISACHABIBIMWENYEKUJIBUMASWALIKWAQURANOTHMANMAALIM #kisachakusikitisha #ramadhani #mawaidharamadhani #qurannasunah #maishayamtume #mawaidhayakifo Matakwa ya Allah ni tuisome Qur’ani ili atuongoze na atuingize peponi. Ndugu Muislamu Tusomeni Qur’an na Tuwasomeshe watoto wetu ili waweze Kuinukia katika kuipenda Qur'ani,na Vile vile tuwahifadhishe watoto wetu wakiwa wadogo kwani kuhifadhi kwa udogoni ndio Wataweza kuhifadhi vizuri na kubaki ndani ya nyoyo zao. kwani kuhifadhi udogoni ni kama kuchonga kwenye jiwe. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ فاطر:29-30 [Hakika wanaosoma hiki Kitabu cha Allah na wakasimamisha swala na wakatoa kwa mali yao tulizowapa kwa siri na dhahiri, wanatarajia biashara isiofilisika, na hakika Allah atawalipa awaongeze, kwani yeye mweyekusamehe saana na ni mwenye kushukuriwa ] [Faatir: 29-30] Na mke wa Mtume ‘Aisha akazidi kutufafanulia akisema: ‘Kusoma kwa Qur’ani kunatafautiana, kuna anayesoma hodari. Hivyo, thawabu zake ni nyingi kiasi cha kutangamana na Malaika na anayesoma akigongagonga atapata malipo mara mbili. Vilevile Abi Umama akamwambia amemsikia Mtume akisema: اقرءوا القرآن فإنه يأتي يوم القيامة شفيعا لأصحابه] رواه مسلم] [Someni Qur’an, itakufaa siku ya Qiyama kuwaombea shufaa.] [Imepokewa na Muslim.] Haya yote ni fadhila za Qur’an na fadhila za kusoma Qur’an. Mtume wetu ﷺ alimuusia Abu Said akimwambia: أُوصِيكَ بِتَقْوَى اللَّهِ ، فَإِنَّهُ رَأْسُ كُلِّ شَيْءٍ ، وَعَلَيْكَ بِالْجِهَادِ ، فَإِنَّهُ رَهْبَانِيَّةُ الْإِسْلَامِ ، وَعَلَيْكَ بِذِكْرِ اللَّهِ ، وَتِلَاوَةِ الْقُرْآنِ ، فَإِنَّهُ رَوْحُكَ فِي السَّمَاءِ ، وَذِكْرُكَ فِي الْأَرْضِ رواه أحمد [Nakuusia umche Mwenyezi Mungu, kwani hilo ndio kichwa cha kila kitu, na utoke kwenda Jihad kwani hilo ndio daraja kuu la Uislamu na umtaje Mwenyezi Mungu Na kwa wingi, na usome Qur’an ukifanya hivyo roho yako itakuwa mahali pazuri mbinguni na utakuwa na utajo upo ardhini.] [Imepokewa na Ahmad]