У нас вы можете посмотреть бесплатно Maisha ya Korea Kusini - PART 1: Fursa za Elimu na Ajira 🌍 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Je, unajua kuwa Korea Kusini ni moja ya nchi zinazojulikana kwa nidhamu ya kazi, ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia duniani? 🚀 Je, umewahi kujiuliza ni nini kinawafanya vijana kutoka mataifa mbalimbali kuchagua Korea Kusini kwa masomo, kazi na ujasiriamali? 🎓💼 Na je, maisha yakoje kwa Mtanzania anayeishi na kujenga ndoto zake katika nchi hii yenye kasi kubwa ya maendeleo? 🇹🇿🇰🇷 Katika kipindi hiki cha #SogaZaDiaspora, ninazungumza na Zubeda Abdul, Mtanzania anayeishi Korea Kusini ambaye amefanikiwa kusoma, kufanya kazi, na kuanzisha shughuli za ujasiriamali katika mazingira mapya. Anatueleza safari yake ya kujifunza, kukua na kutumia fursa zilizopo — kuanzia elimu, kazi, hadi biashara. Zubeda Abdul pia ni Mjasiriamali anayefanya shughuli za kununua na kusafirisha bidhaa mbalimbali toka Korea Kusini hadi nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania. Kama unahitaji mawasiano yake, anapatikana kupitia kurasa yake ya Instagram: / officialzuby pamoja na namba ya WhatsApp ya +8222802093. Tunazungumzia: 📚 Mfumo wa elimu na nafasi za masomo kwa wageni 💼 Maisha ya kazi na namna ya kujiweka katika soko la ajira 🚀 Fursa za ujasiriamali na ubunifu kwa vijana wa kimataifa 🌍 Mafunzo na uzoefu unaoweza kuwasaidia Watanzania wengine wanaotamani kuchukua hatua kama yake Kama unatafuta msukumo wa kuendeleza taaluma yako, kuboresha ujuzi wako au kujifunza kutoka kwa wenzetu wanaofanikiwa nje ya nchi — basi usikose kutazama video hii hadi mwisho! 🌟 Topics tulizogusia: 00:00 - Karibu Soga za Diaspora 00:13 - Tumtambue Zubeda Abdul 00:38 - Je uliendaje Korea Kusini? 01:01 - Gharama za maisha zikoje Korea Kusini kwa Mwanafunzi? 01:22 - Kwanini hukutaka kutafuta scholarships kwenda kusoma Korea Kusini? 02:22 - Utofauti wa vibali vya makazi kwa wanafunzi wa scholarships na wanaojisomesha wenyewe. 03:30 - Gharama za maisha kwenye miji mikubwa, hasa kwa wanafunzi wanaojisomesha wenyewe. 04:03 - Je vyuo vizuri vinapatikana miji gani nchini Korea? 04:48 - Ushauri kwa wanafunzi wanaojisesha wenyewe juu ya makazi sahihi. 07:23 - Urahisi wa kupata vibali vya kuishi baada ya masomo nchini Korea kusini. 08:51 - Je, unapaswa kubadili aina ya visa baada ya kumaliza masomo na kutaka kufanya kazi au ujasiriamali? 09:43 - Muda wa kupata vibali. Hakuna mlolongo. 10:55 - Ubora wa elimu Korea Kusini vs Tanzania 12:23 - Umuhimu wa lugha ya Kikorea katika kuendesha maisha nchini Korea. 15:05 - Kozi nzuri kusoma nchini Korea kwa lugha ya Kiingereza 16:40 - Ubaguzi wa rangi nchini Korea 💬 Tuambie: Ungependa kujifunza nini zaidi kuhusu maisha ya Watanzania wanaoishi Korea Kusini? 📌 Usisahau ku-subscribe, ku like, na kushare ili kuwahamasisha Watanzania wengine duniani kote. #SogaZaDiaspora #KoreaKusini #Tanzania #Elimu #Ujasiriamali #Fursa #MaishaUghaibuni